Wednesday , 8 February 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Samia ataja sababu za Chadema kurudi kundini
Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataja sababu za Chadema kurudi kundini

Spread the love

 

RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimekubali kushiriki mkutano wa pamoja wa vyama vya siasa Tanzania, kwa kuwa malalamiko yao yamesikilizwa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Rais Samia ametoa kauli hiyo leo Jumanne, tarehe 3 Januari 2023, katika mkutano wake na viongozi wa vyama vya siasa 19, jijini Dar es Salaam.

“Faida yake ni ipi? Matunda yake leo Chadema tunao hapa, wamekuja kwenye mkutano wa vyama sababu wamesikilizwa, wamesema yao tumeyasikia tumezungumza kwamba twendeni boti moja na leo wapo tunakwenda boti moja ndiyo faida ya kuzungumza,” amesema Rais Samia.

Rais Samia amesema “mkaona nchi imetulia tunakwenda kufanya maendeleo hakuna papa papa sababu tumezungumza amani inapatikana, leo nashukuru vyama vyote 19 vilivyopata usajili viko hapa.”

Hata hivyo, Rais Samia amesema haikuwa kazi rahisi Chadema kurudishwa kundini, wakati wa mazungumzo kati yake na ujumbe wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuhusu maridhiano.

“Uko upande wa pili kuna chama kikasema hatuingii humo kuna yetu muyasikilize pembeni , nikapata maoni mengi msiyasikilize hayo nikasema hapana kwa sababu tunataka kujenga taifa moja wacha niwasikilize nikamwambia makamu wangu chukua hiyo kazi naye akachagua wenzie watano upande wa CCM na akamtataka na mwenzie alete watano wamekaa wamezungumza mengi,” amesema Rais Samia na kuongeza:

“Wamezungumza mengi nadhani mpaka ripoti ya mwisho nimepata taarifa wamefanya mikutano sita au saba. Lakini mikutano ya awali haikuwa rahisi ilikuwa vuta nikuvute. Kinana anarudi mwenyekiti kazi nzito, nikamwambia wewe mzazi wa vyama vyote nenda kakae kazungumze akazungumza mpaka Kinana na Mbowe ukiwaweka meza moja wanakaa.”

Akizungumza katika mkutano huo, Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi, amesema kwa mara ya kwanza viongozi wa vyama vyote vya siasa 19 wameshiriki wote.

“Kwa vile sisi kama wanasiasa umetupa upendeleo kuwa tasnia ya kwanza kukutana na wewe mwaka mpya wa 2023. Nipende kusema kwamba hata hadhara ya wanasiasa waliokuwepo hapa kwa mara ya kwanza kwa muda mrefu nikiwa kwenye ofisi ya msajili leo wote wamefika, vyama vyote 19 wamepata kuhuduria. Nishukuru ilikuwa wito wa muda mfupi sana lakini wameweza kufika,” amesema Jaji Mutungi.

Chama cha Chadema kiligomea kushiriki mikutano takribani miwili iliyokutanisha vyama vyote vya siasa kutokana sababu mbalimbali, ambapo katika mkutano wa vyama vya siasa uliofanyikia Desemba 2021, jijini Dodoma, kiligoma kushiriki kikitaka mwenyekiti wake aliyekuwa rumande akikabiliwa na mashtaka ya ugaidi, aachwe huru.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Bunge labaini madudu mfumo ukusanyaji mapato, h’shauri tatu kikaangoni

Spread the love  KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali...

Habari za Siasa

Mkuu wa wilaya ya Rungwe azindua vyumba sita vya madarasa vya thamani ya 64 mil

Spread the love  MKUU wa Wilaya ya Rungwe, Jaffar Haniu amezindua vyumba...

Habari za Siasa

Mbunge afurahia mabilioni ya Samia kutua jimboni

Spread the love  MBUNGE wa Igunga, Nicholas Ngassa ameishukuru Serikali kwa utekelezaji...

Habari za Siasa

PIC yaishauri Serikali kuanzisha mfuko wa uwekezaji kusaidia mashirika ya umma

Spread the love  KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji...

error: Content is protected !!