RAIS wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan amezitaka benki zote nchini zinazotoa mikopo, kupunguza riba ili kutowaumiza wakulima wenye nia ya kuendeleza kilimo cha kibiashara. Anaripoti Isaya Temu, TUDARCo…(endelea).
Hayo ameyasema leo tarehe 8 Agosti 2023 alipokuwa akitembelea katika mabanda mbalimbali katika kilele cha sikukuu ya wakulima Nane Nane katika viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya.
Rais Samia ametoa maelekezo akiwa kwenye banda la Benki ya Stanbic ambapo ameitaka benki hiyo pamoja na zingine kupunguza riba kwenye mikopo.
“Mnajua kuna mabadiliko haya ya hali ya hewa, hivyo mkiwawekea wakulima riba kubwa, unamtundika badala ya kumsaidia, kwa hiyo mvua isiponyesha ni kama kusukumia tu kibao afe, umeshamtundika roho yake pale kwenye riba.. kwa hiyo angalieni sera zenu mrudi chini,” amesema Rais Samia.
Wakati huo huo Rais Samia akiwa kwenye banda la NMB alipewa maelezo na mtoa elimu kuwa wao wameshapunguza riba na kufikia asilimi tisa ili kukuza sekta ya kilimo nchini.
Awali, Rais Samia amepokea maelezo kutoka kwa Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe walipokuwa katika banda la Stanbic Bank benki hiyo imekuwa ikitoa mkopo wenye riba ya ya kuanzia asilimia 10 kwenda juu.
Leave a comment