Friday , 3 May 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Rais Ruto amuonya Raila Odinga
Kimataifa

Rais Ruto amuonya Raila Odinga

Spread the love

 

RAIS wa Kenya, William Ruto, amemtaka kiongozi wa upinzani nchini humo, Raila Odinga, kuacha mpango wake wa kuitisha maandamano ya siku tatu mfululizo, la sivyo Serikali yake itakabiliana naye. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Kiongozi huyo wa Kenya amemtaka Raila asitishe harakati zake zinazoweza kusababisha damu za wakenya kumwagika ili apate mamlaka, badala yake asubiri Uchaguzi Mkuu wa taifa hilo unaotarajiwa kufanyika 2027.

“Uchaguzi umekwisha. huwezi kutafuta uongozi kwa kutumia damu na kuharibu mali yao.. Nisikilize kwa makini huwezi kutumia njia zisizo za kisheria, zisizo za kikatiba kutafuta mamlaka nchini Kenya, subiri 2027. Nitakushinda tena,” amesema Ruto.

Rais Ruto ameweka bayana kuwa, safari hii hayuko tayari kumwita mezani Raila kwa ajili ya mazungumzo.

Raila alitangaza kuitisha maandamano hayo wiki ijayo kuanzia Jumatano hadi Ijumaa, akidai watatekeleza suala hilo hadi pale Serikaliya Rais Ruto itakaposikiliza na kufanyia kazi maoni ya wananchi kuhusu maboresho ya Sheria mpya ya fedha kwa lengo la kushusha gharama za maisha.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Mwanamke Rwanda ataka kupambana tena na Kagame

Spread the loveKIONGOZI wa kihistoria wa upinzani nchini Rwanda, Victoire Ingabire Umuhoza,...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

error: Content is protected !!