Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Mwinyi awaita wadau katika mapambano ukatili wa kijinsia
Habari za Siasa

Rais Mwinyi awaita wadau katika mapambano ukatili wa kijinsia

Spread the love

 

RAIS wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi, ameziomba Asasi za Kiraia  na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGO’s), ziunge mkono juhudi za Serikali yake katika kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar … (endelea).

Rais Mwinyi ametoa wito huo leo Jumatano, tarehe 28 Julai 2021, akizindua mfumo wa kanzi data ya kukusanya takwimu za vitendo vya ukatili wa kijinsia, visiwani Zanzibar.

Mwenyekiti huyo wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, amesema Serikali yake inahitaji mchango wa wadau katika kukabiliana na vitendo hivyo, ambavyo vimeshamiri visiwani humo katika siku za hivi karibuni.

“Suala hili la udhalilishaji wa wanawake na watoto linawagusa wadau wengi.  Zipo taasisi za serikali zinahusika nalo lakini pia zipo taasisi binafsi.  Tunahitaji nguvu ya pamoja sote kukabiliana na hili,” amesema Rais Mwinyi.

Uzinduzi wa mfumo huo umeenda sambamba na kongamano la harakati za kutokomeza vitendo vya udhalilishaji Zanzibar, lililohudhuriwa na wadau mbalimbali wa kutetea haki za binadamu.

 

Lulu Ng’wanakilala

Akizungumza katika kongamano hilo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Legal Services Facility (LSF),  nchini Tanzania, Lulu Ng’wanakilala ameiomba Serikali ya Zanzibar, iweke mikakati ya kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia,  ikiwemo mijadala na makongamano  kwa kushirikisha wadau  wa maendeleo ya jamii visiwani humo.

Ng’wanakilala ameiomba Serikali hiyo, pamoja na wadau wa kutetea haki za binadamu, watumie fursa ya kongamano hilo, kupata muarobaini wa vitendo vya ukatili wa kijinsia, vinavyoongoza kuathiri kuwanawake.

“Kongamano hili liwe fursa kwa wadau, katika kuweka mikakati thabiti dhidi ya ukatili wa kijinsia,”  amesema Ng’wanakilala.

Mtendaji huyo wa LSF amesema, kumekuwa na vitendo vya ukatili wa kijinsia, hasa  kwa wanawake na watoto.

“Ripoti yetu inaonyesha katika kila matukio manne ya ukatili yaliyoripotiwa na wanawake yalihusisha unyanyasaji wa kijinsia, ambapo visa vyote vilivyoripotiwa vinakadiriwa kufikia asilimia 26.5 kwa mwaka 2020,”

“Hii inaonesha changamoto kubwa ya upatikanaji haki, hasa kwa wanawake wanaokutana na ukatili kwenye shughuli za uchumi na nyumbani,” amesema Ng’wanakilala.

Ng’wanakilala amesema, LSF itaendelea kushirikiana na Serikali na wadau wengine wa kutetea haki za binadamu, ili kulinda  haki za wanawake na makundi maalumu, yanayoongoza kwa kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia.

“LSF kama mdau katika sekta ya upatikanaji haki na msaada wa kisheria, tutaendelea na ushirikiano na  kuwa tunaamini katika nguvu ya pamoja kwenye kujenga mazingira rafiki kwa wanawake wote na kutetea kundi  la watoto,” ameongeza Ng’wanakilala.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Jumuiya ya Wanawake Wanasheria Zanzibar (ZAFELA), Jamila Mahmoud Juma, amesema  hali ya vitendo vya udhalilishaji katika jamii bado ipo kwa kiasi kikubwa,  ikilinganishwa na zamani licha ya jitihada mbalimbali kufanyika.

“Tumegundua kuwa ili kuwasaidia wanawake wasidhalilike ni lazima wawezeshwe kiuchumi.  Hivyo sisi kama ZAFELA tunatoa mafunzo ya uwezeshaji kiuchumi kwa wanawake ili waweze kujitegemea.  Vilevile, tunatoa elimu na msaada wa kisheria kwa wanawake wanakumbana na vitendo vya udhalilishaji,” amesema Jamila.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

error: Content is protected !!