May 29, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Lamine ampewa mkono wa kwaheri Yanga

Lamine Moro, Nahodha wa Yanga

Spread the love

 

KLABU ya Yanga imeachana rasmi na mlinzi wake wa kati, ambaye pia alikuwa nahodha wa kikosi hicho, Lamine Moro baada ya makubaliano ya pande zote mbili. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Lamine ameacha na klabu yake hiyo baada ya kuitumikia katika kipindi cha miaka miwili.

Taarifa kutoka iliyotolewa na klabu ya Yanga, imeeleza kuwa ndoa ya wawili hao imevunjika ramsi kwa kufikia muafaka wa pande zote mbili na kumtakia kila la heri.

Mchezaji huyo anaachana na Yanga baada ya sintofahamu ya muda mrefu na kufanya kukosa baadhi ya michezo ya Ligi Kuu, kutokana na utovu wa nidhamu.

Kuondoka kwa Lamine kutaifanya klabu ya Yanga kuingia sokoni kwa ajili ya kutafuta mlinzi mwingine wa kati katika dirisha hili kubwa la usajili.

error: Content is protected !!