June 30, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Bakwata yaitisha dua kudhibiti Korona, yahimiza barakoa ibadani

Katibu wa Baraza la Ulamaa la Bakwata, Sheikh Hassan Chizenga

Spread the love

 

BARAZA Kuu la Waislamu wa Tanzania (Bakwata), limewaagiza Maimamu wake kufanya dua maalumu wakati wa swala, ili Mungu aliepushe Taifa na janga la Ugonjwa wa Korona (UVIKO-19). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam …n(endelea).

Maelekezo hayo yametolewa leo Jumatano na Katibu wa Baraza la Ulamaa la Bakwata, Sheikh Hassan Chizenga, akizungumza na wanahabari mkoani Dar es Salaam.

“Baraza la Ulamaa linawaagiza Maimamu wote nchini, kufanya dua mbalimbali, pamoja na kusoma dua ya Kunuti katika kila swala, kumbembeleza Mola wetu alipeperushie mbali gonjwa hili,” amesema Sheikh Chizenga.

Mbali na kuitisha dua hiyo, Bakwata imetoa masharti kwa waumini wake, ili kukabiliana na maambukizi ya UVIKO-19, wakati wa ibada.

“Ibada ya Mungu ndiyo jambo muhimu kuliko yote ulimwenguni, kwa kuwa ndiyo kiunganishi baina ya mwanadamu na Mungu, hivyo havina budi kuendelea huku tukizingatia miko ya wizara ya afya, kama ilivyotolewa,” amesema Sheikh Chizenga.

Sheikh Chizenga ametaja masharti hayo ni, uwekaji vifaa vya kunawia mikono, ikiwemo maji safi yanayo tiririka na sabuni au vitakasa mikono.

Kila muumini kuvaa barakoa wakati wa ibada, pamoja na kukaa umbali wa mita moja kati ya mtu na mtu.

“Watu ambao kitaalamu wametambuliwa kuwa ni rahisi kuambukizwa gonjwa la UVIKO-19, kama wa kisukari, shinikizo la damu, kansa na kadhalika, wanashauriwa kujiweka mbali na mikusanyiko mikubwa ili kujilinda,” amesema Sheikh Chizenga.

error: Content is protected !!