RAIS wa Zanzibar, Dk. Hussein Mwinyi, amemteua Jaji mstaafu wa Mahakama ya Rufaa, Mbarouk Salim Mbarouk kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Shule ya Sheria Zanzibar. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar … (endelea).
Taarifa ya Mhandisi Zena Said, Katibu Mkuu Kiongozi wa Zanzibar imesema, uteuzi wa Jaji Mbarouk umeanza leo Jumamosi, tarehe 17 Julai 2021.

Jaji Mbarouk ni Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Leave a comment