Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Magufuli ‘amparula’ hadharani Mbunge wake
Habari za Siasa

Rais Magufuli ‘amparula’ hadharani Mbunge wake

Rais John Magufuli
Spread the love

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli, amewaagiza viongozi wa Manispaa na Mkoa wa Morogoro, kuwaacha wafanya biashara ndogondogo kuendelea kufanya biashara zao katika eneo la kituo cha mabasi cha Msamvu, anaadika Mwandishi Wetu.

Rais Magufuli ametoa agizo hilo leo baada ya msafara wake uliokuwa ukitokea Dodoma kuelekea jijini Dar es Salaam kusimamishwa na wananchi wa eneo hilo kwa lengo la kuelezea kero zao za kufukuzwa na Manispaa katika maeneo yao yaliyopo kituo cha mabasi, baada ya kituo hicho kujengwa upya.

Baada ya kusikiliza kero zao Rais amemuagiza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro SACP, Ulrich Matei, kuhakikisha Askari Mgambo hawawasumbui wafanya biashara hao, na kutafuta utaratibu mzuri kwa ajili yao ili kuepusha vurugu.

Wakati huo huo Rais amewataka watu wote walionunua viwanda mbalimbali katika Mkoa huo kuvirejesha Serikalini kama wameshindwa kuviendeleza, ili wapewe wawekezaji wanaoweza kuviendeleza na kuzalisha ajira.

“Ninarudia wito wangu niliokwisha kuutoa huko nyuma, kwamba wenye viwanda hapa Morogoro ambao wameshindwa kuviendesha, na leo nataja akiwemo Mbunge wa hapa wa Chama Cha Mapinduzi CCM ambaye alibinafsishwa viwanda vingi, kama ameshindwa kuviendesha, avirejeshe ili tuwape watu wengine kwa sababu vijana wanakosa ajira, nazungumza kwa uwazi kwa sababu msema kweli ni mpenzi wa Mungu.” amesema Rais Magufuli.

Pia Rais amewapongeza wakulima wa mazao mkoani humo kwa kuongeza uzalishaji wa mazao na amewataja wakulima wa Wilaya ya Kilosa kwa kuongeza uzalishaji kutoka asilimia 42 msimu uliopita hadi kufikia asilimia 82 katika msimu huu.

Kuhusu mradi wa ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa (Standard Gauge), Rais Magufuli ametoa wito kwa wananchi wa Morogoro kujitokeza kupata ajira wakati wa ujenzi, lakini amewataka waliojenga katika hifadhi ya reli kuondoa majengo yao kwa hiari.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

error: Content is protected !!