August 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

CCM Arusha kuanza kutibuana wiki hii

Spread the love

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Arusha, kinatarajia kuanza kazi ya kuchuja majina ya wanachama wake walioomba ridhaa ya kuteuliwa kugombea nafasi mbalimbali za uongozi, anaandika Mwandishi Wetu

Katibu wa chama hicho wilayani hapa, Ramadhani Dallo, amesema jana wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.

Amesema waliochukua fomu za kuomba kugombea uenyekiti wa wilaya ni wanachama 27, lakini waliorejesha walikuwa 23.

Aliongeza kuwa wanachama 35 walichukua fomu kugombea nafasi ya Katibu wa Siasa na Uenezi, lakini waliorudisha ni 34 wakati waliochukua fomu kuombea nafasi za ujumbe wa mkutano mkuu taifa walikukwa 67 na walioresha fomu walikuwa 59.

Kwa upande wa nafasi za ujumbe wa halmashauri ya CCM Wilaya waliochukua fomu walikuwa 90 na wote walirejesha wakati nafasi za ujumbe za halmashauri kuu ya CCM Mkoa waliochukua fomu walikuwa na 41 na wote walirejesha.

error: Content is protected !!