Tuesday , 5 December 2023
Home Habari Mchanganyiko Qwihaya waipiga ‘tafu’ Polisi vita ya corona
Habari Mchanganyiko

Qwihaya waipiga ‘tafu’ Polisi vita ya corona

Meneja wa Kampuni ya Qwihaya, Ntibwa Mjema akizungumza na waandishi wa habari
Spread the love

KAMPUNI inayozalisha nguzo za umeme ya Qwihaya General Enterprise Co Ltd imelikumbuka jeshi la Polisi mjini Mafinga, wilayani Mfindi Mkoa wa Iringa kwa kutoka vifaa vya kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona vinavyo sababisha ugonjwa wa covid 19. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Msaada huo ni mwendelezo wa ziara ya Qwihaya katika kukabidhi vifaa hivyo maeneo mbalimbali na tayari zaidi ya Sh65 milioni zimetumika kwa kazi hiyo tangu janga hilo lianze.

Akikabidhi msaada huo, Meneja wa Qwihaya, Ntibwa Mjema amesema kampuni hiyo imeamua kushiriki kwa vitendo vita dhidi ya corona ikiunga mkono jitihada za Serikali katika kupambana.

“Tumetoa vitakasa mikono, barakoa na sabuni ili wenzetu polisi wanapotekeleza majukumu yao wawe kwenye mazingira salama,” amesema Mjema.

Kwa upande wake, Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Mufindi, Abichi Masanga aliishukuru kampuni hiyo na kuziomba kampuni nyingizi ziige mfano huo.

“Tunashukuru kwa huu msaada na bado tunahitaji msaada mwingine, hapa wanakuja raia wengi na watuhumiwa wakiwa hapa wanahitaji barakoa na sanitaiza kwa hiyo, mahitaji makubwa” amesema Kamanda Masanga.

Kwa sasa kampuni ya Qwihaya inamilikiwa na Mzalendo, ndugu Leonard Mahenda ina viwanda vya kuzalisha nguzo za umeme katika mikoa ya Iringa na Kigoma huku mkakati ukiwa kumaliza uhaba wa bidhaa hiyo ambayo awali ilikuwa ikiingizwa kutoka nje ya nchi unamalizika.

Qwihaya umeme unawaka vijijini kama mijini

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

TMA yaagizwa kutangaza mafanikio yao kikanda, kimataifa

Spread the love  KATIBU Mkuu Wizara ya Uchukuzi, Prof. Godius Kahyarara ameiagiza...

Habari Mchanganyiko

NMB yasaidia waathirika wa mafuriko, maporomoko Hanang

Spread the loveWaathirika wa maporomoko ya tope Wilayani Hanang, mkoani Manyara, waliopoteza...

Habari Mchanganyiko

TPF-NET Arusha yaonya jamii ya wafugaji zinazoendeleza ukatili wa watoto na wanawake

Spread the love  MTANDAO wa Polisi wanawake wa Arusha kuelekea siku 12...

Habari Mchanganyiko

Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Greyhorse zasaini mkataba wa bil.7.4

Spread the loveTAASISI ya Mwalimu Nyerere (MNF) imesaini mkataba wa miaka 10...

error: Content is protected !!