July 26, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Walimu 18,181 wameajiriwa 2015/20 – Serikali

Prof. Joyce Ndalichako, Waziri wa Elimu

Spread the love

SERIKALI imeeleza, kuanzia mwaka 2015 mpaka 2020, sekta ya elimu imeajiri walimu 18,181. Shule ya Msingi 10,666, sekondari 7,218 na mafundi sanifu maabara 297. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Rashid alitaka kujua, lini na mkakati gani serikali imeweka ili kukabili upungufu wa walimu kwenye shule zake.

“Sekta ya elimu nchini inakabiliwa na uhaba wa walimu, Je, serikali imeweka mkakati gani wa kuziba pengo hilo la uhaba wa walimu,” amehoji Rashid Abdallah Shangazi, Mbunge wa Mlalo leo tarehe 14 Mei 2020.

Wizara imeeleza, “serikali itaendelea kuajiri walimu katika Sekta ya elimu kwa kadri ya upatikanaji wa rasilimali fedha,” imeeleza Wizara ya Elimu.

Pia Tunza Issa Malipo (Mbunge wa Viti Maalum – Chadema), amehoji idadi ya shule za sekondari zinazofundisha somo la TEHAMA.

Wizara hiyo imeeleza kwamba, Shule za Sekondari zinazofundisha somo la TEHAMA nchini ni 188. Shule 47 ni za serikali na 141 ni binafsi.

“Serikali inaendelea kuandaa mazingira wezeshi na kuimarisha eneo la rasilimali watu, kwa kuongeza walimu waliosomea Somo la TEHAMA.

“Imeendelea kuziwezesha Shule za Sekondari kuwa na vifaa vya

kisasa vya TEHAMA, kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ili kuziwezesha shule nyingi kufundisha somo hilo,” imeeleza wizara.

error: Content is protected !!