Tuesday , 5 December 2023
Home Habari Mchanganyiko Corona inavyowatesa wafanyabiashara kuelekea Sikukuu ya Eid
Habari Mchanganyiko

Corona inavyowatesa wafanyabiashara kuelekea Sikukuu ya Eid

Spread the love

BAADHI ya Wafanyabiashara  katika Soko la Kariakoo jijini Dar es Salaam, wameeleza namna janga la mlipuko wa virusi vya Corona, lilivyoathiri biashara zao. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Mlipuko wa virusi vya corona unaathiri biashara nyingi nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, hasa kufuatia hatua za serikali ulimwenguni kupiga marufuku shughuli  zenye mikusanyiko ya watu wengi, na hata wengine kufikia hatua ya kuzuia kabisa watu wasitoke nje ya makazi yao.

Marufuku hizo zimepelelea wananchi wengi kusimamisha shughuli zao wa kiuchumi kwa ajili ya kutekeleza marufuku hizo sambamba na kujikinga na maambukizi ya maambukizi ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu, inayosababishwa na virusi vya Corona (covid 19).

Wakizungumza na MwanaHALISI Online katika nyakati tofauti leo tarehe 13 Mei 2020, baadhi ya wafanyabiashara hao wamesema mwenendo wa biashara zao umekuwa wa kusua sua, kutokana na ubaha wa wateja.

Wamesema uhaba huo wa wateja unatokana na hofu dhidi ya Covid-19, ambao walio wengi hushindwa kufika katika soko hilo, kwa kuhofia kuambukizwa, kupitia mikusanyiko ya watu wengi.

Pia, wamesema kwamba, watu wengi kwa sasa hali zao za kiuchumi zimeyumba, kutokana na janga hilo, hali inayopelekea kushindwa kufanya manunuzi ya mahitaji mbalimbali.

Moris Kimaro, mfanyabiashara wa viatu vya watoto katika Soko la Kariakoo, amesema katika kipindi hiki cha maandalizi kuelekea Siku Kuu ya Eid el Fitri, biashara zao zina sua sua, tofauti na miaka ya nyuma kabla ya mlipuko wa Corona.

Kimaro amedai kuwa, kipindi hiki cha msimu wa siku kuu, hupata wateja wengi wanaonunua viatu kwa ajili ya watoto wao, lakini mwitkio wa msimu wa mwaka huu, umekuwa mdogo kutokana na uhaba wa wateja.

“Biashara imekwua ngumu sana, yaani wakati mwingine unaweza kuja hapa,  tangu asubuhi hadi jioni unafunga hujauza hata 50,000, na wakati mwingine unaondoka patupu,” amesema Kimaro.

Sadick Fidelis, Mfanyabiashara wa nguo za watoto sokoni hapo, amesema mwenendo wa biashara hauridhishi kutokana na mlipuko wa corona.

“Biashara ngumu hususan kwa wamachinga wanaofanya biashara ndogondogo, baadhi yao wamefunga biashara wamekimbia soko sababu biashara hamna mitaji imekata. Mtu anakuja kuanzia asubuhi hadi jioni hapati kitu, hata hela ya futari inamshinda,” amesema Fidelis.

Mwanahamisi Rashid, mfanyabiashara wa matunda sokoni hapo, amesema biashara ngumu tofauti na kipindi kabla ya mlipuko wa virusi vya Corona.

“Zamani ulikuwa unauza vizuri lakini sasa hivi unaokoteza wateja, wanakuja kidogo nahisi kwa sababu ya kuhoifia kuambukizwa corona,” amesema Mwanahamisi.

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

TMA yaagizwa kutangaza mafanikio yao kikanda, kimataifa

Spread the love  KATIBU Mkuu Wizara ya Uchukuzi, Prof. Godius Kahyarara ameiagiza...

Habari Mchanganyiko

NMB yasaidia waathirika wa mafuriko, maporomoko Hanang

Spread the loveWaathirika wa maporomoko ya tope Wilayani Hanang, mkoani Manyara, waliopoteza...

Habari Mchanganyiko

TPF-NET Arusha yaonya jamii ya wafugaji zinazoendeleza ukatili wa watoto na wanawake

Spread the love  MTANDAO wa Polisi wanawake wa Arusha kuelekea siku 12...

Habari Mchanganyiko

Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Greyhorse zasaini mkataba wa bil.7.4

Spread the loveTAASISI ya Mwalimu Nyerere (MNF) imesaini mkataba wa miaka 10...

error: Content is protected !!