Friday , 26 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa ‘Putin anaugua kansa’
Kimataifa

‘Putin anaugua kansa’

Rais wa Urusi, Vladimir Putin
Spread the love

 

MAJASUSI kutoka nchi tano za barani Ulaya, Australia na Amerika Kaskazini, wamedai Rais wa Urusi, Vladimir Putin anapatiwa matibabu ya saratani hali iliyomsababishia kupata ugonjwa kupoteza fahamu au kumbukumbu (dementia).

Pia inadaiwa kuwa matibabu hayo yanaweza kumsababishia ugonjwa wa kutetemeka (Parkinson) au ugonjwa wa hasira za mara kwa mara. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Majasusi hao kutoka nchi za Australia, Marekani, Canada, New Zealand na Uingereza waliopo nchini Urusi, wamehusianisha madhara ya magonjwa hayo na uamuzi wa Rais huyo wa Urusi kuivamia Ukraine tarehe 24 Februari, mwaka huu.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Maily la nchini Uingereza, majasusi hao wamesema katika ripoti yao kwamba tabia isiyo ya kawaida inayooneshwa na Putin pamoja na dalili nyingine, ndizo zinazowaaminisha kuwa anaugua saratani.

Licha ya kwamba hawakufafanua ni saratani ya aina gani, ila wameeleza kuwa matibabu mbadala ya saratani (steroid) yameonesha Rais Putin akiwa na uvimbe usio wa kawaida shingoni tofauti na picha za miezi kadhaa iliyopita.

Pia waliongeza kuwa kutokana na matibabu hayo, Putin mwenye umri wa miaka 69, ameendelea kujiweka mbali na wageni wanaomtembelea Ikulu ya Kremlin kama ilivyoonekana pindi Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron alipomtembelea hivi karibuni.

Aidha, ripoti hiyo ilienda mbali na kudai kuwa hivi karibuni Putin amewasweka mahabusu baadhi ya makamanda ambao wameshindwa kufikia malengo ya vikosi vya katika uvamizi wa Ukraine.

Hayo yanajiri wakati nchi za Muungano wa Kijeshi wa mataifa ya Ulaya, Marekani, Canada na Uturuki (NATO) yakiendelea kuibua propaganda katika vita kati ya Urusi na Ukraine licha ya kwamba hadi sasa yamesita kutoa msaada wa kijeshi kwa Ukraine na hata kuinyima nchi hiyo kuwa mwanachama wa muungano huo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!