Saturday , 20 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Polisi yapiga marufuku ving’ora, vimulimuli
Habari Mchanganyiko

Polisi yapiga marufuku ving’ora, vimulimuli

Spread the love

 

JESHI la Polisi Tanzania, kupitia Kikosi cha Usalama Barabarani limepiga marufuku matumizi ya ving’ora na vimulimuli, kwa watumiaji wa magari binafsi. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Marufuku hiyo imepigwa leo Jumatatu, tarehe 14 Machi 2022 na Kamanda wa Polisi, Kikosi cha Usalama Barabarani, SACP Wilbroad Mutafungwa.

Taarifa ya Kamanda Mutafungwa imesema, kama kuna mtu ana dharura anahitaji kutumia ving’ora, anatakiwa kuomba kibali kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi au Jeshi la Polisi, ambapo kama ataruhusiwa atasindikizwa kwa kutumia ving’ora.

“Tunazidi kuwakumbusha kwamba, magari yanayopaswa kutumia ving’ora na vimulimuli kwa dharura ni magari ya kubeba wagonjwa (Ambulances), zimamoto, ya vyombo vya ulinzi na usalama na magari mengine yaliyopatiwa kibali na Waziri wa Mambo ya Nchi na kutangazwa kwenye gazeti la Serikali,” imesema taarifa ya Kamanda Mutafungwa.

Kamanda wa Polisi, Kikosi cha Usalama Barabarani, SACP Wilbroad Mutafungwa

Aidha, taarifa ya Kamanda Mutafungwa imesema, kikosi chake kinaendelea kufanya doria katika mikoa yote nchini, kukamata watu watakaokiuka marufuku hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, magari yaliyokamatwa yakiwa na vimulimuli na ving’ora visivyo rasmi ni 1,527, ikiwemo magari madogo na malori.

Pikipiki na bajaji zilizokamatwa zikiwa na vifaa hivyo ni 1,358 huku magari ya watu binafsi na Serikali yaliyokamatwa yakitumia namba bandia ni 73.

Gari la wagonjwa

“Kwa kuzingatia kwamba majukumu ya Jeshi la Polisi KIKOSI CHA Usalama Barabarani ni kusimamia utekelezaji wa sheria na kanuni za usalama barabarani, tumeanza kufanya doria na misako katika barabara kuu za mikoa yote Tanzania Bara,” imesema taarifa ya Kamanda Mutafungwa na kuongeza:

“Na kufanikiwa kukamata magari, pikipi na bajaji ambayo wamiliki na madereva wake wamekwenda kinyume na matakwa ya sheria.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

error: Content is protected !!