Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Profesa Kabudi aomba Morogoro iwe jiji
Habari Mchanganyiko

Profesa Kabudi aomba Morogoro iwe jiji

Prof. Palamagamba Kabudi
Spread the love

MBUNGE wa jimbo la Kilosa mkoani Morogoro, Profesa Palamagamba Kabudi, ameomba mbele ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo kuupandisha hadhi Manispaa ya Morogoro iweze kuwa jiji. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Profesa Kabudi ametoa ombi hilo leo Jumapili tarehe 5 Februari 2023, wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wa kuadhimisha kilele cha miaka 46 ya CCM uliofanyika viwanja vya Sabasaba mkoani Morogoro.

Pia Prof. Kabudi pia ameomba kuwepo kwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa huku akiieleza kuwa pamoja na ukubwa wa mkoa huo hakuna hospitali yenye hadhi yake.

“Mkoa huu ni mkubwa hauna hospitali inayolingana na mkoa wa Morogoro, tano tunaomba mji wa Morogoro kuwa jiji, la sita wewe umeutembea mkoa wa Morogoro wote tunaomba bajeti ya TARURA iongezwe maradufu,” amesema Kabudi.

Katika hatua nyingine Prof. Kabudi amekiomba chama chake kutimiza ahadi za Ilani ya Uchaguzi yam waka 2020-2025 ambapo amesema iliahidi kujenga na kukarabati reli ya Kilosa-Kidatu.

“Katika kutekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi  tunaomba ukurasa wa 94 Ibara ya 59 inazungumza kukarabati na kufufua reli ya kutoka Kilosa kwenda Kidatu, tunaomba reli hiyo ifufuliwe ili sasa Kilosa iwe ndiyo wilaya inayounganisha reli tatu, reli ya sasa, reli ya kisasa na reli ya Mlimba kule TAZARA-Profesa Palamagamba Kabudi, Mbunge wa Kilosa

Amesema reli hiyo ikikamilika Mlimba, Kidatu na Kilosa zitakuwa vituo vya usafirishaji “na sisi tunaomba ikiwezekana reli ya Kilosa-Kidatu isiwe meter gauge iwe Cap Gauge ili sasa treni zikitoka Mlimba zije hadi Kilosa na ikiwa Cap gauge ni rahisi pia kuingia kwenye SGR.”

Aidha ameomba ujenzi wa barabara za kuunganisha mkoa wa Mororgoro na mikoa mingine, mkoa wa Njombe mkoa wa Ruvuma na mkoa wa Lindi na Mkoa wa Tanga na wilaya za Mlimba, Malinyi, Ulanga, Mvomero, kwa maana ya barabara ya Turiani-Msiha.

“Hizi ni barabara ambazo zipo ndani ya Ilani ya Chama cha Mapinduzi na moja umeipita wakati wa ziara yako barabara ya Kilosa-Mikumi na barabara ya Chanzulu- Merera,” amesema.

Aidha ameahidi kuwa mkoa huo utaongoza katika kura za urais katika uchaguzi mkuu wa 2025 kama ambavyo iliongoza mwka 2020.

2 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

error: Content is protected !!