Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Polisi wagwa vyeti kwa wamiliki wa silaha za jadi
Habari Mchanganyiko

Polisi wagwa vyeti kwa wamiliki wa silaha za jadi

Spread the love

 

KAMISHNA Msaidizi wa Jeshi la Polisi ACP Theopista Malya leo Oktoba 07, 2023 amegawa vyeti kwa wamiliki wa silaha za kiraia tukio hilo limefanyika katika ukumbi wa mikutano Wanji eneo la Mpemba mjini Tunduma wilaya ya Momba na mkoani Songwe. Anaripoti Ibrahim Yassin, Songwe … (endelea).

Sambamba na zoezi hilo la ugawaji wa vyeti kamanda Mallya aliwataka wamiliki hao wa siraha ambao ni wafanyabiashara na wakulima wakubwa mkoani hapa kuweka kamera za ulinzi (Cctv) Katika maeneo yao ya biashara na Kuajiri walinzi waliopitia mafunzo ya kijeshi na sio wazee, ni lazima walinzi wa mali zao wavae sare na wawe wawili, ikiwa ni pamoja na wenye uweledi wa kufanya kazi za ulinzi.

Aidha Kamanda wa polisi mkoa wa Songwe ameongeza kwa kusema mafunzo ya ulengaji wa shabaha kwa wamiliki wa silaha za kiraia yatakua endelevu pia amewaagiza wakuu wa polisi wa wilaya mkoa wa Songwe kuhakikisha wamiliki wote wa silaha wanapata mafunzo maalum ambayo yatasaidia kuwakumbusha matumizi sahihi ya silaha.

Kwa upande wawamiliki wa silaha za kiraia mkoani Songwe wamelishukuru jeshi la polisi kwa mafunzo waliyoyapata na wamehaidi watatekekeza yale yote waliyofundishwa kwenye mafunzo hayo yaliyofunguliwa rasmi Agosti 7, 2023 na kufungwa Agosti 12, 2023 na hatimaye leo kugaiwa vyeti

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NEMC yatoa elimu matumizi sahihi ya zebaki kwa wachimbaji

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Oryx gesi yagawa mitungi, majiko 100 kwa waandishi wa habari Dar

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gesi Tanzania imegawa mitungi 100 ya gesi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari MchanganyikoMichezo

Wanamichezo Mei Mosi wachangia wahitaji vitu vya mil. 11.5

Spread the loveWanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha...

error: Content is protected !!