Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Madereva Tunduma waridhishwa na usalama wa maegesho, waomba yatanuliwe
Habari Mchanganyiko

Madereva Tunduma waridhishwa na usalama wa maegesho, waomba yatanuliwe

Spread the love

 

MADEREVA wa magari makubwa ya mazigo (Malori) wanaovuka mpaka wa Tunduma kwenda nchi za kusini mwa afrika (SADC) wameiomba halmashauri ya wilaya mji Tunduma wilayani Momba mkoani Songwe kuutanua mradi wa maegesho kuongeza tija. Anaripoti Ibrahim Yassin, Songwe … (endelea) .

Wakizungumza leo tarehe Octoba 8/ 2013 kwenye mradi huo,wamesema wameridhishwa na usalama na huduma zilizopo kwenye paking hiyo ila wanaomba mradi huo utanuliwe kwani madereva wengi wanakimbilia kupaki eneo hilo kikwazo ni ufivyu wa eneo.

Bashiru Kassim ni dereva wa Lori kutoka kampuni ya mafuta ya Afroil amesema toka mradi huo uanzishwe wamekuwa na amani kwani usalama wa magari yao ukilinganisha na maeneo mengine ambayo usalama ya magari yao ni mdogo kutokana na wizi.

Plus Njeluis dereva amesema Tunduma wamebuni mradi mzuri uliovutia madereva wengi kupaki eneo hilo huku wengine wakikosa nafasi hivyo also based wahusika wautanue mradi huo kuvutia madereva wengi, imefikia hatua hata kugeuza gari inakuwa shida.

Mkurugennzi mtendaji wa halmashauri hiyo Philimon Magesa amesema walibuni mradi huo kwa na kuujanga kwa gharama ya Tsh. 1,700,000,000.00. Makusanyo kwa mwezi ni Tsh. 5,900,000.00 na kwa mwaka 70,800,000.00.

Amesema waliamua kujenga  kwa kuwa Tunduma ni mji wa kibiashara asilimia 75 ya bidhaa zinazovuka bandari ya Dar es salaam yanavuka kwenye mpaka huo kupitia Malori, hivyo kutokana na kuwa na wateja wengi wamejipanga kutanua mradi kwani eneo walilonalo bado ni kubwa.

Amesema mradi huo ulianza mchakato wake mwaka 2021 hadi sasa umekamilika na unafanya kazi na ni moja ya vyanzo 35 vya mapato vinavyopelekea Tunduma kukusanya zaidi ya Bilioni 11 kwa mwaka na kushika namba 2 kitaifa kwa makusanyo wakiongozwa na manispaa ya Ilala.

Ameongeza kuwa mbali na kuwa ni chanzo cha mapato ya halmashauri, pia ni fursa za kiuchumi kwa mama lishe wanaopika vyakula na bodaboda na bajaji wanaobeba madereva kuwapeleka maeneo mbali mbali ikiwemo ofisi za uhamiaji na TRA kufanya taratibu za kuvuka mpaka.

Amesema mbali na mradi huo pia wanajenga mradi mungine ambao ni nyumba ya kulala wageni na mgahawa (Restouse na Restaurant ), Ili madereva watakapopaki magari kwenye maegesho hayo, waweze kula na kulala sehemu hiyo hiyo itakayowawezesha kufanya mambo yao ya kimpaka kiurahisi.

“Mradi wa maegesho tumejenga kwa Tshs,1.700,000,000.00,na mradi wa Restouse na restaurant tumejenga kwa Milioni 500 za mapato ya ndani upo hatua za mwisho kukamilika, na miradi ipo eneo moja nyuma ya ofisi za halmashauri ya mji Tunduma “amesema Garigo.

Hasan Seif dereva wa Lori amesema wameondokana na usumbufu wa kupaki magari hovyo kwa sasa wanapaki wanalala na kulala chakula sehemu moja na kuwa uongozi wa halmashauri wamebuni kitu kizuri.

Merry Mtafya mama lishe na mkazi wa eneo hilo la Chapwa amesema uwepo wa mradi huo umewapa fursa za kupika vyakula, kuuza matunda, na kujipatia kipato kinachokidhi kuendesha maisha yao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Equity Bank yaendelea kusotea mabilioni ya fedha mahakama rufani

Spread the loveBENKI za Equity ya Tanzania na Kenya, zimeendelea kupambana mahakamani...

Habari Mchanganyiko

NEMC yatoa elimu matumizi sahihi ya zebaki kwa wachimbaji

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Oryx gesi yagawa mitungi, majiko 100 kwa waandishi wa habari Dar

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gesi Tanzania imegawa mitungi 100 ya gesi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

error: Content is protected !!