Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Dk Wanga atoa somo matumizi bora ya misitu
Habari Mchanganyiko

Dk Wanga atoa somo matumizi bora ya misitu

Spread the love

 

KATIBU Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC), Dk Godwill Wanga ametoa rai kwa wadau wa uhifadhi misitu, akiwemo serikali, sekta binafsi na wananchi kuzingatia matumizi bora ya misitu, kwa kuhakikisha kinachovunwa ni kile ambacho kipo kwenye mpango wa matumizi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Dk Wanga ametoa rai hiyo jana wakati akifunga warsha ya wadau wa misitu iliyofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Utalii (NCT) jijini Dar es Salaam, kwa kuandaliwa na Program ya Kuendeleza Mnyororo wa Thamani wa Mazao ya Misitu (FORVAC), ambapo aliweka wazi kuwa sekta hiyo ni muhimu katika kukuza uchumi na huduma za jamii.

Amesema dhamira ya Rais Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha rasilimali misitu inakuwa na mnyororo wa thamani kuanzia ngazi ya chini, hivyo ili kufikia huko ni wajibu wa kula mdau kushiriki katika utunzaji rasilimali hiyo muhimu.

Katibu huyo amesema rasilimali misitu ina faida nyingi kwenye jamii ikiwemo utunzaji mazingira, uzalishaji wa bishaa mbalimbali, kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na nyingine, hivyo ni vema kila mdau kushiriki kuiendeleza.

“Program ya FORVAC imewezesha vijiji 39 katika wilaya 12 kuwa na matumzi bora ya ardhi, kutenga na kuhifadhi misitu 71, kuunda Kamati 39 za Maliasili (VNRC), kuunda mipango ya usimamizi misitu, kutangaza misitu 16 kwenye gazeti la serikali na kuanisha miradi 67 ya kiuchumi ambayo imeongeza mnyororo wa thamani wa mazao ya misitu,” amesema.

Aidha, Dk Wanga ameishauri serikali na wadau kuachana na dhana ya kutumia Miti ya Mninga na Mkongo katika mahitaji yao ya thamani za ofisi, kwani tafiti zimeonesha kuwa kuna zaidi ya miti 1,600 ambayo inafaa kwa kazi hiyo.

Katibu huyo ameitaka Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kuwasiliana na Mamlaka ya Usimamizi wa Ununuzi wa Umma (PPRA), GPSA na wadau wengine kuhakikisha miti yene sifa sawa na hiyo inapata kipaumbele kwenye taasisi za umma.

Amesema kwa upande wa vijiji ni muhimu kumilikishwa misitu, ili kuhakikishi kuwa inalindwa na kuwa endelevu na kuzitaka taasisi zingine ziige kwa FORVAC.

“Wataalamu wa misitu mnapaswa kufanya kazi karibu na kamati za vijiji na wanavijiji ndipo dhamira hii ya Serikali kupitia mradi huu wa FORVAC itaweza kuzaa matunda,” amesema.

Dk Wanga amesema TNBC itaendelea kushirikiana na wizara na taasisi zote kuhakikisha misitu inachangia pato la taifa, hali ambayo itawezesha malengo ya Rais Samia kutamani uchumi shirikishi yanatimia.

Mratibu wa FORVAC, James Nshare amesema program hiyo ambayo ilianza 2018 imeweza kuongeza mnyororo wa thamani kwa rasilima ambayo inawazunguma.

“FORVAC imewezesha wananchi wa vijiji kutambua thamani ya misitu baada ya kuunganishwa katika mnyororo wa thamani, kinyume cha hapo misitu asili ambayo ipo vijijini ingekuwa katika hali mbaya,” amesema.

Nshare amesema kupitia program hiyo wamewezesha wananchi kutumia rasilimali misitu kwa zaidi ya asilimia 66, kutoka asilimia 30 ambayo ilikuwa awali, hivyo mikakati yao ni kuhakikisha uhifadhi kwa njia hiyo unaendelea.

Amesema FORVAC imenufaisha wananchi zaidi 10,000 moja kwa moja katika mikoa Tanga, Lindi na Ruvuma, huku makundi maalum yakipewa kipaumbele.

“Tunaposema FORVAC inagusa mnyororo wa thamani ni kwamba vijiji vimejenga zahanati, shule, wamekata bima za afya na huduma nyingine, hivyo maisha ya wananchi yanakuwa rahisi kama anavyotaka Rais Samia,” amesema.

Mtaribu huyo amesema kupitia FORVAC vijana na wakina mama wamweza kuaminika na kupewa mikopo ya halmashauri, hivyo kuongeza mtaji wao.

Kwa upande Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijiji vya Hifadhi ya Misitu Kilwa (UVIHIMIKI), Ally Kinunga amesema FORVAC imewaletea mapinduzi ya kiuchumi kwa muda mchache, hivyo kuiomba Serikali iendeleze program hiyo.

Kinunga amesema vijiji vingi vina hali mbaya ya uhifadhi, hivyo jitihada zinahitajika kuhakikisha program kama hizo zinakuwa endelevu.

“Mfano Wilaya ya Kilwa ina vijiji 90, ila ni vijiji 11 ambavyo vina hifadhi ya misitu, ina maana misitu mingine haina usimamizi endelevu na hii sio Kilwa tu, ukienda Ruangwa, Liwale, Nachingwea, Tunduru, Namtumbo na kwingineko ni hivyo hivyo,” amesema.

Mwenyekiti huyo amesema wakati umefika kwa serikali kuweka uzito kwenye uhifadhi, kama inavyofanya kwenye sekta ya afya, miundombunu, kilimo, maji na huduma zingine.

“Kasi ya mabadiliko ya tabianchi ni kubwa sana, hatua zinahitajika kuchukuliwa kwa haraka, kunusuru misitu yetu na nchi kwa ujumla,” amesema.

Ofisa Mtendaji wa kijiji cha Limamu amesema FORVAC imekuwa neema kwa vijiji husika ambapo program inatekelezwa.

“Wakina mama wameweza kujiajiri kupitia FORVAC, mimi kama kiongozi wa kijiji naomba Serikali ipambane program iwe endelevu, kwani hitaji ni kubwa,” anasema.

Amesema kupitia program hiyo uhifadhi wa mazingira umeweza kuimarika na kuboreshwa, huku jamii ikiwa mlinzi na rafiki wa misitu.

Naye Mfanyanishara wa Mazao ya Misitu, Thomas Masikini Program ya FORVAC imeweza kuongeza ubora na thamani ya rasilimali za misitu zinazozalishwa vijijini na kuziomba taasisi nyingine ziweze kuendeleza.

Amesema FORVAC imeweza kusaidia vijiji mashine za kisasa ambazo zinawezesha kuzalisha rasilimali misitu katika njia bora, kuwa na uhakika wa soko.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NEMC yatoa elimu matumizi sahihi ya zebaki kwa wachimbaji

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Oryx gesi yagawa mitungi, majiko 100 kwa waandishi wa habari Dar

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gesi Tanzania imegawa mitungi 100 ya gesi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari MchanganyikoMichezo

Wanamichezo Mei Mosi wachangia wahitaji vitu vya mil. 11.5

Spread the loveWanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha...

error: Content is protected !!