Monday , 11 December 2023
Home Kitengo Michezo Lavaud agonga kolabo ya kibabe na Tiwa Savage…
Michezo

Lavaud agonga kolabo ya kibabe na Tiwa Savage…

Spread the love

STAA wa kike kwenye uwezo mkubwa katika kuimba na kutunga, Lavaud amerejea kwa kishindo baada ya kuachia singo kali inayokwenda kwa jina la “Roll on Me” – ikiwa kwenye mitandao ya Saint & Citizen Music. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Katika singo hiyo, amewashirikisha mastaa kadhaa wa muziki Afrika wakiwemo, Tiwa Savage,
Patoranking, Reekado Banks na Kanis.

Kwa hakika mastaa hao wamezidi kuinogesha singo hiyo na kuifanya yenye ladha ya kipekee.

Kwenye “Roll on Me” kuna mikono ya maprodyuza wakali, kama Kel-P, ambaye amepata kufanya kazi na wasanii Burna Boy, Wizkid, Rema na Trakmatik.

Akizungumzia traki hiyo, Lavaud anasema: “Nimefurahi sana kufanya kazi na wasanii wakubwa wenye uwezo na vipaji vya aina yake, lakini zaidi timu nzima ya utayarishaji. Nimependa jinsi tulivyoonyesha tamaduni na mila zetu za Kiafrika kwenye wimbo huo ambazo kwa hakika zimeongeza uzuri na upekee wa singo hiyo.”

Naye Tiwa Savage amesema: “Pale wasanii wanapokutana pamoja, kama hivi, kitu fulani cha kuvutia hutokea… na ndivyo ilivyokuwa.

“Huu wimbo ni mzuri na wa kipekee, nimefurahishwa na mchango wa kila mmoja wetu katika hii kazi.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Pesa ipo huku Meridianbet, beti sasa

Spread the love  WIKIENDI inaishia leo hii jaman kama bado hujasuka mkeka...

Michezo

Wenzako wameshakuwa mamilionea hapa wewe unasubiri nini?

Spread the love  WIKIENDI imefika na ukiachana na mvua za Dar es...

Michezo

Manchester City vichwa chini Ligi Kuu England

Spread the love MABINGWA watetezi wa ligi kuu ya Uingereza klabu yaManchester City...

Michezo

Piga mkwanja wa kutosha katika usiku wa kibabe kati ya Man United vs Chelsea

Spread the love USIKU wa leo katika dimba la Old Trafford utapigwa mchezowa...

error: Content is protected !!