Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Polisi Arusha wamkamata Wakili Madeleka
Habari MchanganyikoTangulizi

Polisi Arusha wamkamata Wakili Madeleka

Madeleka
Spread the love

WAKILI wa kujitegemea nchini, Peter Madeleka amekamatwa na Jeshi la polisi mkoani Arusha katika Kituo Jumuishi cha utoaji haki baada ya kutoka Mahakama Kuu Kanda ya Arusha. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Madeleka amekamatwa muda mfupi baada ya kujifungia ndani ya chumba cha Mahakama (chember court) cha Jaji Aisha Bade kwa zaidi ya dakika 30.

Awali Jaji Bade ndiye aliyetoa maamuzi katika kesi ya Wakili Madeleka ya kupinga makubaliano ya kukiri kosa ‘Plea Bargain’ kati yake na Ofisi ya Mwendesha Mashtaka (DPP).

Kabla ya kukamatwa Madeleka leo Jumatatu aliandika kwenye akaunti yake ya Twitter kwamba Maofisa wa Jeshi la Polisi wanamuwinda nje ya Mahakama Kuu Kanda ya Arusha ili wamkamate baada ya kufutiwa Plea Bargaining na Jaji Aisha Bade wa Mahakama hiyo.

Plea Bargaining hiyo iliyotokana na kesi ya uhujumu uchumi Na. 81 ya mwaka 2019 ambapo alilipa Sh. 2 milioni.

Madeleka aliueleza mtandao wa MwanaHALISI kuwa bado hajatoka kwenye chumba cha Mahakama akihofia kukamatwa.

Dakika chache baadae Madeleka aliandika kuwa, “Hukumu iliyosomwa leo na Mahakama Kuu ya Tanzania Arusha mbele ya Jaji Bade licha ya kufuta Plea bargain kati ya DPP na Madeleka, ilikuwa imeshajukana kwa polisi na DPP kabla ya kusomwa na Mahakama ikasaidia mazingira ya mimi kukamatwa”.

Hata hivyo, baada ya kufika Wakili wa Madeleka katika mahakama hiyo, Simon Mbwambo na wanahabari Wakili Madeleka alitoka ndani ya chumba cha Mahakama na baadae kukamatwa na polisi.

Wakili wa Madeleka, Simon Mbwambo amesema hajui kosa la mteja zake, zaidi ya kuwaona polisi wakimkata na kumpeleka Ofisi ya RCO (Mkuu wa Upelelezi Mkoa Arusha) kwa mahojiano alisema na kuongeza kuwa “Labda wanataka kuanza upya kusikiliza kesi hii ya leo.”

MwanaHALISI limemtafuta Kamanda wa Polisi mkoani Arusha ACP Justine Masejo kwa njia ya simu bila mafanikio.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

error: Content is protected !!