Sunday , 19 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Pigo jingine: Bernard Membe afariki dunia
Habari za Siasa

Pigo jingine: Bernard Membe afariki dunia

Marehemu Bernard Kamilius Membe
Spread the love

 

ALIYEKUWA Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa, katika utawala wa Rais Jakaya Kikwete, Bernard Kamilius Membe, amefariki dunia, asubuhi ya leo, 12 Mei 2023. Anaripoti Saed Kubenea, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa kutoka kwa mmoja wa wanafamilia ambaye hakupenda kutajwa jina lake, amethibitisha kuwa Membe amefariki dunia katika hospitali ya Kairuki, iliyopo Mikocheni, jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa mtoa taarifa huyo, mwanasiasa huyo alipelekwa hospitalini hapo kutokea nyumbani kwake Mikocheni, jana majira ya saa tatu usiku baada ya kulalamika kuwa hajisikii vizuri.

“Ni kweli kwamba Baba yetu, Bernard Membe amefariki dunia. Alianza kuumwa jana usiku na tukampeleka hospitali. Ni bahati mbaya kwamba leo asubuhi ameaga dunia,” alieleza mwanafamilia huyo.

Membe aliyezaliwa tarehe 9 Novemba 1953, katika Kijiji cha Rondo, Chiponda, alikuwa mmoja wa mawaziri wandamizi katika serikali ya Kikwete, hadi kutajwa kuwa angekuwa mrithi wake katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Alikuwa mtoto wa pili kati wa watoto saba wa familia ya Kamillius Anthony Ntachile na Cecilia John Membe.

Aliteuliwa kuwa waziri wa mambo ya nje, mwaka 2007 na alishika wadhifa huo, hadi mwaka 2015. Amekuwa mbunge wa Mtama katika Bunge la Jamhuri, kuanzia mwaka 2000 hadi 2015, akitokea ubalozi wa Tanzania nchini Canada.

Alihudumu kwenye wadhifa wa afisa mwandamizi  wa ubalozi kwa zaidi wa miaka tisa; kabla ya kupelekwa Kanada, alikuwa akifanya kazi Idara ya Usalama wa taifa (TISS).

Mwaka 2015 alijitosa katika kinyang’anyiro cha mbio za urais, kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), lakini hakuweza kupenya.

Mwaka 2018 alilaumiwa na “kulaaniwa sana” na  gazeti la Tanzanite, kwamba alijaribu kumzuia rais John Magufuli asipewe nafasi ya kugombea tena nafasi hiyo, katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

Membe alifungua kesi ya kuchafuliwa jina lake, dhidi ya gazeti hilo, mkurugenzi wake, Cyprian Musiba na mhariri wake.

Alishinda shauri hilo, ambapo Oktoba 2021, Mahakama Kuu, imeamuru mwanasiasa huyo, kulipwa na gazeti hilo, mhariri wake na mmiliki wake – Cyprian Musiba – kumlipa fidia ya zaidi ya Sh. 9 bilioni.

Mwaka 2019 Membe aliitwa mbele ya Kamati Kuu (CC) ya CCM, ili kuhojiwa kuhusu mashtaka ya kula njama dhidi ya Magufuli. Akaishia kufukuzwa uanachama wa chama hicho.

Baada ya kufukuzwa ndani ya CCM, mwanasiasa huyo maarufu, alihamia chama cha ACT – Wazalendo, ambako alifanywa kuwa mgombea urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

Katika kipindi chote cha utawala wa Magufuli, Membe ndiye aliyebaki katika historia ya kuwa mwanasiasa pekee aliyeweza kutoka hadharani kumkosoa kiongozi huyo aliyekuwa anaogopwa na kila mtu nchini Tanzania.

Hivyo basi, wadadisi wa mambo wanasema, “hakuna shaka kuwa kifo chake, kitakuwa pigo kubwa kwa siasa za Tanzania na demokrasia yake.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Wakili Mwabukusi anusurika kufungiwa, asema hatarudi nyuma

Spread the loveWAKILI Boniface Mwabukusi amesema kuwa hatorudi nyuma kuwatetea Watanzania na...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

RC Chongolo atangaza ‘vita’ kwa wanaovusha wageni kinyemela

Spread the loveKATIKA kulinda usalama wa nchi kupitia mpaka wa Songwe, Mkuu...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

RUWASA yachongewa, yateketeza mamilioni kwa maji yenye magadi

Spread the loveSAKATA la ukosefu wa maji wilayani Momba mkoani Songwe limezidi...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Lissu akabidhiwa gari lake, aomba msaada wa matengenezo

Spread the loveMakamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, Tundu Lissu leo Ijumaa amekabidhiwa...

error: Content is protected !!