Saturday , 27 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Balile, Kalinaki waula jumuiya ya wahariri EAC
Habari Mchanganyiko

Balile, Kalinaki waula jumuiya ya wahariri EAC

Spread the love

JUMUIYA ya Wahariri Afrika Mashariki imemchagua Daniel Kalinaki wa Jukwaa la Wahariri Uganda kuwa Rais wa Jumuiya ya Wahariri Afrika Mashariki kuanzia Mei 12, 2023, ambapo ataongoza kwa mwaka mmoja. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Deodatus Balile, ambaye ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), naye amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wahariri Afrika Mashariki, kuanzia Mei, 2024 hadi Mei, 2025.

Kwa mujibu wa Katiba ya Jumuiya ya Wahariri Afrika Mashariki, katika kipindi cha mwaka mmoja ambacho Balile anasubiri kushika wadhifa wa Urais wa Jumuiya ya Wahariri Afrika Mashariki mwezi Mei 2024, kwa sasa atakuwa ni Naibu Rais wa Jumuiya ya Wahariri ya Afrika Mashariki.

Daniel Kalinaki

Umoja wa Wahariri wa Afrika Mashariki Katiba yake inatoa nafasi ya kumwandaa kiongozi wake ajaye kwa mwaka mmoja baada ya kumchagua kama sehemu ya maandalizi ya kuifahamu vyema kazi yake kabla ya kushika madaraka hayo rasmi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!