November 29, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Othman, ujenzi wa Chama imara silaha kuu ya kushinda uchaguzi 2025

Makamu Mwenyekiti Chama cha ACT-Wazalendo, Othman Massoud Othman

Spread the love

 

MAKAMU Mwenyekiti Chama cha ACT-Wazalendo, Othman Massoud Othman amewataka wanachama kuimarisha chama chao ili kuwa imara zaidi hatimae kuibuka na ushindi katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 kwa nafasi ya urais na nyinginezo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar … (endelea).

Othman ambaye pia na Makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar ameyasema hayo leo tarehe 24 Septemba, 2022 katika ziara maalumu ya ujenzi wa Chama hicho katika maeneo mbalimbali mkoa wa Mjini magharibi Unguja.

Othman ameambatana na viongozi mbalimbali wa chama na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi.

Alisema anaamini kuwa kupitia harakati hizo za ujenzi wa Chama zitaleta tija na zitawafanya wao wawe washindi wa uchaguzi mkuu mwaka 2025 ukizingatia yalio mengi yameahidiwa bila kutekelezwa huku wananchi wakiendelea kulalamika ugumu wa maisha.

Alieleza kuwa kukosekana kwa uwajibikaji madhubuti kwenye Serikali kumewafanya wanachi kukata tamaa na wengi wao kupoteza matumaini na Serikali inayoongozwa na CCM.

Sambamba na hayo Othman alisema ili hali ya ugumu wa maisha iweze kuondoka au kupungua wananchi hawana budi kukiunga mkono chama cha ACT-Wazalendo kwani ndio chama pekee chenye dira ya kweli na kuongoza nchi bila ya ubaguzi wa aina yoyote hile.

Akizungumzia kuhusu uwepo wao Serikali ni kutokana na deni kubwa ambalo wamepewa na wananchi tangu mtangulizi wake Marehem Maalim Seif Sharif Hamad hivyo hawataacha kutetea maslahi ya walio wengi kwa njia ya halali akimini ipo siku haki itasimama.

Makamu Mwenyekiti Chama cha ACT-Wazalendo, Othman Massoud Othman

‘’Najua tumekua tukipitia changamoto mbali mbali kwenye kila hatua ila ninachotaka muelewe ni kwamba changamoto hizi tunazoendelea kuzipata ni dhahiri kuwa mafanikio yapo karibu na hatupaswi kukata tamaa’’aliongezea.

Awali mjumbe wa kamati kuu Chama cha ACT Wazalendo Ismail Jussa alisema haoni dhamira safi ya uendeshaji wa Serikali ukizingatia baadhi ya wanaoteuliwa ndio wanaofanya ubadhirifu na wizi wa fedha za Umma.

Jussa alitolea mfano ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) iliotolewa hivi karibuni na kuibua taarifa ya kupotea kwa mabilioni ya fedha na kusema wahusika ni watu ambao wameajiriwa au kupewa teuzi kwa kuaminiwa na wenye mamlaka na ndio hao hao waliochukua fedha hizo.

Alisema hatua ilipoanza kuchukuliwa kwa watu waliolezwa kubainika kufanya makosa hayo ni sawa na geresha kwa kuwa wapo wengi na wenye nafasi kubwa zaidi wanaendelea kufanya kuliko hayo huku wakifumbiwa macho kama kwamba wanayoyafanya ni yahalali.

Mjumbe huyo wa kamati kuu ya chama cha ACT-Wazalendo alionesha kusikitishwa na baadhi ya viongozi kubeba mamlaka makubwa wakiikosesha Serikali mamilioni ya fedha ambayo yangepatikana kupitia kodi.

Akitolea mfano alisema katika siku za hivi karibuni kupitia gazeti la Nipashe iliripotiwa taarifa ya kiongozi mmoja ambae pia ni mfanyabiashara alielta gari lake visiwani hapa na kutakiwa kulipia ushuru milioni mia tatu cha kushangaza mkurugenzi wa ZIPA, Shariff Ali Sharif aliandika barua ya kuomba msamaha wa kodi kama gari ya mradi wakati ni gari binafsi ya kutembelea.

‘’Tunaamini taarifa ile ina ukweli mtupu maana hadi leo hii si Mkurugenzi wa ZAIPA wala mwingine yoyote aliyetoka hadharani na kukanusha, tunashangaa hadi sasa Mkurugenzi huyu yupo madarakani licha ya kuikosesha Serikali mapato’’ aliongezea.

error: Content is protected !!