Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Makala & Uchambuzi Nyalandu asimulia mkasa wake na polisi, Takukuru
Makala & Uchambuzi

Nyalandu asimulia mkasa wake na polisi, Takukuru

Lazaro Nyalandu
Spread the love

NAWASHUKURU sana wote walioguswa na mkasa ulionisibu katika saa ya kujaribiwa kwangu mnamo majira ya 8:30 mchana Jumatatu, tarehe 27 Mei 2019. Anaandika Lazaro Nyalandu … (endelea).

Tuliwasili kijijini Itaja, Wilayani Singida kuongea na viongizi wa vijiji na vitongoji Kata ya Itaja kuhusu zoezi linaloendelea nchi nzima la chama chetu kuwatambua na kuwaandikisha wanachama wetu. Jumla ya washiriki walioorodheshwa katika daftari la mahudhurio siku hiyo walikua watu 29.

Kama ilivyoripotiwa, kikao chetu cha ndani, kilivamiwa na watu ambao hatukuwafahamu, wakiwa na silaha na kuamrisha mimi, pamoja wenzangu wawili (David Jumbe na Mwenyekiti wa CHADEMA Kata ya Itaja, ndugu Peter) tuondoke nao.

Sote tulipatwa na mshtuko mkubwa, na hatukupewa utambulisho wala sababu ya kutolewa kwenye kikao na kuchukuliwa na watu wenye silaha mithili ya wahalifu na kutiwa nguvuni, huku wote tuliokuwa nao wakiwa wamepigwa bumbuwazi la sintofahamu.

Watu waliotuchukua walikuwa watano na walikuwa wamejaa katika gari moja aina ya Rav 4 nyeupe, na waliamrisha gari langu aina ya Ford Ranger litumike na wao wakiwa wametufuata kwa nyuma hadi nje ya Benki ya NBC Singida, ambako waliagiza tuingie ofisi ya Takukuru Mkoa wa Singida.

Walimchukua kila moja wetu katika chumba tofauti na kutuhoji juu ya uhalali wa kikao hicho cha CHADEMA, na kudai kuwa kulikuwa na harufu ya rushwa. Baada ya mahojiano, walitupeleka katika kituo kikuu cha Polisi Singida, na muda mfupi baadae tukasikia taarifa ya Takukuru Singida kuwa wao wamejiridhisha hapakuwa na tatizo na wametukabidhi mamlaka ya Polisi.

Polisi walitufanyia mahojiano mengine, kila mmoja wetu katika chumba tofauti, na kutujulisha kuwa wao hawakuwa na neno lolote juu yetu, ispokuwa tukifanya kikao chochote watataka tutoe taarifa kwa OCD Singida, na wakasema tupatiwe dhamana ili turudi kesho yake, Jumanne na kuripoti polisi na Takukuru, (endapo wao Takukuru watakuwa na neno). Tulipopewa dhamana usiku huo, ilikuja AMRI kwamba dhamana hiyo ifutwe, na tukalazwa katika rumande ya Central Police Singida hadi kesho yake.

Siku ya Jumanne, tarehe 28 Mei 2019, tulipatiwa dhamana (mimi kwa wadhamini watatu kwa Sh milioni 5 kila mmoja, na Afisa wa Polisi OCD akaruhusu dhamana hiyo kuwa ya maneno, au ahadi endapo watuhumiwa hawataonekana kuripoti kama ilivyo amri)

Siku ya Jumatano, tarehe 29 Mei 2019,  tulirudi kuripoti Polisi kama ilivyo amriwa katika hati ya dhamana, majira ya saa 2 asubuhi, na Mkuu wa Polisi OCD Singida akaamuru tuendee kudhaminiwa kwa dhamana ile ile hadi Ijumaa, tarehe 31 Mei 2019,  saa 2.00 asubuhi.

Tukiwa tunajiandaa kutoka, Maafisa kutoka Takukuru waliwasili Makao Makuu Polisi kwa OCD Singida na kuamrisha tupelekwe Ofisi ya Takukuru Mkoa wa Singida kwa maelekezo mapya, ambako tuliamriwa kupata tena upya wadhamini moja moja kwa kwa bond ya sh milioni tano kila mmoja wetu, na kuamriwa kuripoti Tarehe 19 June 2019.

Uonevu huu ni dhambi mbele za Mungu, na wanadamu. CHADEMA na vyama vingine vyote vya upinzani wamewekwa katika hali ya mashaka na mateso, na tunatishiwa usalama wetu na kuwekewa mipango lukuki ya kututungia na kutubambikizia kesi.

Hakika, haki huinua Taifa na wote wenye mamlaka, waone fahari kutenda mema. Kwa nilichokipitia siku hizi chache, nawasihi sana CHADEMA na upinzani kwa ujumla wake, siku tutakapo shinda na kushika dola, tusiwafanyie wana CCM au watu wengine mateso kama haya, kwakuwa, yatupasa tuushinde ubaya kwa wema.

Lazaro Nyalandu

Mwanachama, CHADEMA

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaMakala & Uchambuzi

Kanda ya Ziwa yaonyesha NMB inavyosaidia afya ya mama na mtoto

Spread the loveMafanikio inayozidi kupata Tanzania katika kupunguza vifo vya mama na...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

‘Mwanapekee’ wa Rais Samia: Atabadili nini Arusha?

Spread the loveMAPEMA wiki hii, baadhi ya viongozi walioapishwa na Rais Samia...

Habari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Kipunguni waihoji serikali, ziko wapi fedha za fidia?

Spread the loveWATU wanaodai kwamba serikali ya Chama Cha Mapinduzi ni sikivu,...

Habari za SiasaMakala & UchambuziTangulizi

Askofu Bagonza: Tusichonganishwe; tusichokozane na tusikufuru

Spread the loveJOTO la chaguzi linapanda kila siku hapa nchini. Upo umuhimu...

error: Content is protected !!