Tuesday , 16 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Serikali yamjibu Nape kuhusu ATCL
Habari za Siasa

Serikali yamjibu Nape kuhusu ATCL

ATCL Dreamliner
Spread the love

TATIZO la ndege za Shirika la Ndege nchini (ATCL) kuchelewa kuanza safari zake, leo tarehe 30 Mei 2019 bungeni limeibuliwa na Nape Nnauye, Mbunge wa Mtama. Anaripoti Mwanidishi Wetu … (endelea).

Nape ameihoji serikali kwamba, kumekuwepo na tatizo la ndege kuchelewa kuanza safari zake na wakati mwingine bila abiria kupewa taarifa yoyote na kwamba, nini chanzo chake.

“Kumekuwepo na ucheleweshwaji wa kuanza kwa safari za ndege za ATCL na wakati mwingine muda husogezwa mbele, nini kimekuwa kikichangia jambo hili?” amehoji Nape.

Atashasta Nditiye, Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano ameeleza kuwa, tatizo hilo lemekuwa likishughulikiwa na kuwa, kwa sasa kukiwa na ucheleweshwaji, abiria hupewa taarifa.

Nditiye amefafanua kuwa, tayari wamefanya mabadiliko makubwa huku wakiendelea kulikabila tatizo hilo ambalo sasa limepungua.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Samia arejesha mikopo ya 10%, bilioni 227.96 zatengwa

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amerejesha utaratibu wa utoaji mikopo...

Habari za Siasa

Rais Samia amfariji mjane wa Musa Abdulrahman

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan leo Jumanne amempa pole Mwanakheri Mussa...

Habari za Siasa

Nape: Wanasiasa, wanahabari, wafanyabiashara mteteeni Samia

Spread the loveWaziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano,...

Habari za Siasa

CAG: TAWA imegawa vibali vya uwindaji bila idhini ya waziri

Spread the loveRIPOTI ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali...

error: Content is protected !!