Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko NMB yazipiga jeki shule sita mkoani Ruvuma
Habari Mchanganyiko

NMB yazipiga jeki shule sita mkoani Ruvuma

Spread the love

BENKI ya NMB imekabidhi madawati yenye thamani ya zaidi ya Sh 25 milioni kwa shule sita mkoani Ruvuma ikiwa ni utekelezaji wa dhamira ya benki hiyo ya kuchangia uboreshaji wa sekta ya elimu nchini. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Shule zilizonufaika na msaada huo ni pamoja na shule za msingi Kiburangoma, Legele, Lipuma Londoni na Mkuzo za Manispaa ya Songea pamoja na Shule ya Msingi Mateteleka ya Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.

Akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi msaada huo iliyofanyika katika Shule ya Msingi Kiburangoma jana Jumatatu, Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kusini, Faraja Ng’ingo alibainisha kuwa msaada huo pamoja na kuboresha mazingira ya wanafunzi kujisomea unalenga kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita katika kuboresha sekta ya Elimu.

Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof Aldof Mkenda (kushoto) akimsikiliza Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB ,Ruth Zaipuna alipomtembelea waziri huyo ofisini kwake Jijini Dodoma jana.

Ng’ingo alibainisha kuwa Sekta ya Elimu ni miongoni mwa vipaumbele vya benki hiyo katika mkakati wake kabambe wa Uwajibikaji kwa Jamii (CSI) huku akisisitiza kuwa ni Benki ya NMB itaendela kushirikiana na wadau wote ikiwemo Serikali katika kutatua changamoto zinazoikabili jamii wanayoihudumia.

“Sisi kama benki ya NMB tunaamini kuwa elimu ni ufunguo wa maisha. Kwa kulitambua hili, sekta ya elimu ni miongoni mwa vipaumbele vyetu na kwa miaka mingi sasa tumekuwa tukijitoa kuchangia maboresho ya sekta hii muhimu. Nina furaha kuwa leo tunakabidhi madawati kwa shule sita mkoani Ruvuma na nimatumaini yangu kuwa msaada wetu utakuwa chachu ya ufaulu kwa shule hizi sita,”alisema.

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo aliipongeza benki ya NMB kwa msaada huo mkubwa kwa wananchi wa Ruvuma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Prof. Joyce Ndalichako (kushoto) akijadiliana jambo na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna alipomtembelea Ofisini kwake Jijini Dodoma jana

Kanali Thomas alisema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dk Samia Suluhu Hassan imejenga miundombinu muhimu ya sekta za elimu na afya na kuwapongeza wadau wengine ikiwemo benki ya NMB kwa kujitokeza kuunga mkono jitohada za Serikali.

“Huu ni mfano wa kuigwa. Natumia fursa hii kuipongeza benki ya NMB ya kuendelea kuchangia shughuli za maendelo za Serikali. Natoa rai kwa wadau wengine mkoani Ruvuma kuiga mfano huu wa kuchangia maendeleo,” alisema.

Awali Mkuu wa Wilaya ya Songea Kapenjama Ndile aliishukuru banki ya NMB kwa kupunguza changamoto ya madawati na meza katika shule za msingi na sekondari Manispaa ya Songea.

Alibainisha kuwa katika shule za msingi zilizopo Manispaa ya Songea kuna upungufu wa madawati 5,863  huku shule za sekondari  za Manispaa ya Songea zikiwa na upungufu wa meza 6,600.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

Habari Mchanganyiko

TUCTA, OSHA wataka kampuni za madini kuiga ubunifu wa GGML

Spread the loveSHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) pamoja na Wakala...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yashiriki maadhimisho Mei Mosi Arusha

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeungana na maelfu ya...

Habari Mchanganyiko

Makonda autaka mgodi kubadilisha maisha ya wana-Geita

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda ametoa wito kwa...

error: Content is protected !!