Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko NMB yazindua kampeni maalumu kufanikisha msimu mpya wa korosho
Habari Mchanganyiko

NMB yazindua kampeni maalumu kufanikisha msimu mpya wa korosho

Spread the love

WAKATI msimu mpya wa korosho mwaka huu ukitarajiwa kuanza rasmi tarehe 14 Oktoba 2022, Benki ya NMB imezindua kampeni ya “Bonge la Mpango – Mchongo wa Kusini” inayolenga kuwahamasisha wakulima kutumia NMB kufanya miamala, kuweka amana na akiba.

Pia benki hiyo imesema iko tayari na ina uwezo kifedha kuhakikisha lengo la msimu huu la uzalishaji wa tani 400,000 wa zao hilo, linafikiwa. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Ahmed Abbas Ahmed (katikati) akimkabidhi kadi ya pikipiki kiongozi wa chama cha msingi kutoka mkoani Mtwara moja ya pikipiki kama ishara ya kuzindua rasmi kampeni ya ‘Bonge la Mpango Mchongo wa kusini’ itakayohusisha vyama vya msingi vya wakulima wa korosho mkoani Mtwara na Lindi. Kushoto ni Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kusini, Janeth Shango na wapili kushoto ni Mkuu wa Idara ya Kilimo Biashara wa benki ya NMB, Isaac Masusu.

Katika kutimiza lengo hilo hiyo, benki hiyo imebainisha utayari wake na mikakati iliyonayo kulisaidia Taifa kupata matokeo chanya kwenye msimu huu wa 2022/23.

Mbali ya mikopo na huduma zake nyingine, NMB pia imepanga kutumia kampeni hiyo maalumu ya kuhamasisha matumizi ya benki na kuufanya msimu huu mpya kuwa wa mafanikio makubwa zaidi kiuzalishaji na kibiashara ikilinganishwa na msimu iliyopita.

Hayo yamebainishwa jana na Mkuu wa Idara ya Kilimo Biashara wa benki hiyo, Isaac Masusu katika Kongamano la Viongozi wa Vyama vya Ushirika wa mkoa wa Mtwara ambapo pamoja na mambo mengine alizindua kampeni hiyo ya “Bonge la Mpango – Mchongo wa Kusini”.

Akizungumza katika kongamano hilo lililolenga kubadilishana mawazo na jinsi ya kuufanikisha msimu huu, alisema kampeni hiyo inawalenga wakulima wa korosho na vyama vya ushirika (AMCOS).

“Ili kuendelea kuhamasisha matumizi ya huduma za Benki ya NMB kwa wakulima na vyama vya ushirika, leo hii tunawaletea kampeni maalum tunayoiita ‘Bonge la Mpango’ na kwa mwaka huu tumekuja na kauli mbiu ya ‘Mchongo wa Kusini’,” Masusu alisema.

“Tumeona ni vyema tukailenga zaidi kanda hii ya kusini kwani tunataka kuendelea kuvihamasisha vyama vya wakulima (AMCOS) pamoja na wakulima hususani katika kipindi hiki cha msimu wa korosho kuendelea kufanya malipo na kuhifadhi fedha zao katika Benki ya NMB kwa usalama zaidi huku wakiendelea kunufaika na huduma zetu zilizo bora na zilizoenea katika maeneo mbalimbali,” kiongozi huyo alibainisha.

Benki hiyo ilizindua kampeni hiyo jana kwenye Kongamano na Viongozi wa Vyama vya Ushirika Mkoani Mtwara ililoliandaa kwa ajili ya kubadilishana mawazo jinsi ya kuufanikisha msimu huu na wadau wa zao hilo.

Masusu alisema pia kongamano hilo limefanyika kwa kutambua ambavyo kilimo cha korosho kimekuwa nguzo muhimu kwa ustawi wa Kanda ya Kusini hususani mikoa ya Lindi na Mtwara lakini pia kwa taifa na hata Benki ya NMB.

“Benki ya NMB inatambua kuwa uchumi wa kanda hii hususani katika mikoa ya Lindi na Mtwara umeegemea zaidi kilimo cha korosho na ndio maana tumekuja katika kipindi hiki ili mbali na kunufaika na kilimo cha korosho, wakulima kupitia AMCOS zao wataweza pia kunufaika zaidi na zawadi wakitumia Benki ya NMB kuhifadhi pesa zao na kuitumia katika kufanya malipo mbalimbali,” alibainisha.

Aidha, alisema kuwa wakulima watakaoitumia NMB wataziwezesha AMCOS zao kushinda zawadi zilizotengwa kwa ajili ya kampeni hiyo ambayo zawadi zake ni pikipiki tano watakazozipata wshindi kwenye droo zitakazofanyika kila baada ya wiki mbili.

Droo yake ya kwanza itafanyika tarehe 28 Oktoba, 2022. Mbali na kuwahamasisha wakulima kuitumia zaidi benki ya NMB kufanya miamala, sababu nyingine za kampeni hiyo ni kuhamasisha amana na kuwasaidia watu kuweka akiba.

Masusu alisema NMB ina uwezo kifedha na iko vizuri kiutendaji pamoja na kujipanga vizuri sokoni kuhakikisha hayo yanafanyika na kampeni ya “Bonge la Mpango – Mchongo wa Kusini” inafanikiwa.

Hiyo inatokana na kuwa na matawi 228 yaliyotapakaa nchi nzima yakisaidiwa kulihudumia taifa na ATMs zaidi ya 800 huku ukwasi wake wa zaidi ya TZS trilioni 8 ukiwa ndiyo mkubwa sana kwenye tasnia.

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Ahmed Abbas Ahmed, alisema kampeni hiyo itasaidia sana kubadilisha maisha ya watu wengi na kutoa mchango mkubwa kwenye uchumi wa korosho wa Mkoa wa Mtwara.

Alisema Bonge la Mpango inaendana na juhudi za serikali za kurasimisha miamala na kuongeza matumizi ya mifumo ya kibenki, vitu ambavyo ni muhimu kwenye utekelezaji wa agenda ya taifa ya kuendeleza huduma jumuishi za kifedha nchini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NEMC yatoa elimu matumizi sahihi ya zebaki kwa wachimbaji

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Oryx gesi yagawa mitungi, majiko 100 kwa waandishi wa habari Dar

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gesi Tanzania imegawa mitungi 100 ya gesi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari MchanganyikoMichezo

Wanamichezo Mei Mosi wachangia wahitaji vitu vya mil. 11.5

Spread the loveWanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha...

error: Content is protected !!