Thursday , 18 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Matokeo mtihani wa uwakili kuchunguzwa, Dk. Mwakyembe akabidhiwa zigo
Habari MchanganyikoTangulizi

Matokeo mtihani wa uwakili kuchunguzwa, Dk. Mwakyembe akabidhiwa zigo

Spread the love

SERIKALI imeunda kamati ya watu saba itakayochunguza sakata la matokeo ya mtihani wa uwakili katika Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo (Law School), kutokana na kile kinachodaiwa kuwa matokeo mabaya katika mtihani uliofanywa mwaka huu. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Akitangaza kamati hiyo leo tarehe 12 Oktoba, jijini Dodoma, Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Damas Ndumbaro amesema kamati hiyo itakayoongozwa na aliyekuwa Waziri wa zamani kwa nyakati tofauti na mwanasheria, Dk Harison Mwakyembe.

Amesema kamati hiyo imepewa siku 30 za kutoa majibu ya sakata hilo.

Hatua hiyo imekuja baada ya kumeibuka mjadala kuhusu kile kinachodaiwa kushuka kwa ufaulu wa mawakili katika taasisi hiyo ya uanasheria kwa vitendo, ambapo iliripotiwa kwa taarifa za wanafunzi kuwa na matokeo mabaya.

Illielezwa kuwa katika mtihani uliofanyika mwaka huu, jumla ya wanafunzi 651 katika mtihani huo, 26 pekee wamefaulu, 342 wametakiwa kurudia baadhi ya masomo huku wengine 265 wakiwa wamefeli.

Aidha, akielezea magumu aliyopitia katika elimu yake ya sheria, Dk. Ndumbaro alisema anakumbuka alipofanyiwa mtihani wa kutafuta uwakili akibaini kuwa mbali ya kuwa alihitimu Chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na kupata Shahada yake ya kwanza, pia alibaini kujua hafahamu sheria kwa undani.

Alisema mawakili wa kujitegemea wenye kampuni za uwakili pia waajiri katika makampuni, mashirika pamoja na raia wanaoawalipa mawakili wanalalamika mapungufu wanayoona kuhusu wanafunzi mawakili wapya.

Aidha, alisisitiza kuwa shule hiyo kuu ya sheria inayo wakufunzi wa kutosha na wenye uweledi wa kutosha.

Alitolea mfano kuwa wapo majaji 81 wakiwamo majaji wastaafu na walipo kazini, mawakili waandamizi wa serikali wanne, mahakimu wakazi, mawakili waandamizi wanaokwenda kuwapika mawakili watarajiwa katika shule hiyo kuu ya Tanzania.

“Hawa majaji, principal state attorney (senior counsel), mahakimu wakaazi, mawakili wanaojitegemea wanauzoefu wa miaka kadhaa,” alisema.

Waziri Ndumbaro alionesha mfano wa majibu ya ajabu ya mawakili watarajiwa waliofanya mitihani na wanaotaka kuwa na leseni ya uwakili.

Aliongeza kuwa watahiniwa hawafai kabisa kuwa mawakili, mahakimu wala wanasheria wa makampuni, mashirika na idara za umma.

WAJUMBE WA KAMATI HAWA HAPA

Kamati imeundwa kufuatia sakata hili la malalamiko ya wadau Dk. Harrison Mwakyembe na Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumu, Sirillius Matupa ambaye alikuwa mshauri wa Rais wa awamu ya nne.

Wengine ni Mwenyekiti Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma Zanzibar, Assaa Ahmad Rashid kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Gloria Kalabamu ambaye ni Makamu wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Alice Edward Mtulo – wakili mwandamizi ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, Mary Stephen Mniwasa ambaye ni Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Soko la hisa Dar es Salaam (DSE) na John John Kaombwe ambaye ni mhitimu juzi kundi la wahitumu awamu ya 33.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!