Tuesday , 7 May 2024
Home Habari Mchanganyiko NMB yaweka historia mpya, yaorodhesha hatifungani soko la mitaji Ulaya
Habari Mchanganyiko

NMB yaweka historia mpya, yaorodhesha hatifungani soko la mitaji Ulaya

Spread the love

Tukiwa tunaadhimisha siku ya wanawake duniani, NMB imeandika historia mpya kwa kuwa Benki ya kwanza Kusini mwa Jangwa la Sahara kuorodhesha hatifungani ya kijinsia katika soko la hisa barani Ulaya. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Hatifungani hiyo inayojulikana kwa jina la ‘Jasiri’ imeorodheshwa leo katika soko la hisa la Luxembourg, moja ya masoko makubwa ya uwekezaji wa mitaji duniani.

Mhazini wa NMB, Aziz Chacha akihutubia katika hafla hiyo.

Hatifungani hiyo ina lengo la kukusanya fedha kwa ajili ya kutoa mikopo kwa biashara ndogo na za kati zinazomilikiwa na wanawake na biashara ambazo bidhaa au huduma zake zinamgusa mwanamke moja kwa moja.

Hadi kufikia Disemba 2022, Sh bilioni 74 zilizokusanywa awali kutoka kwenye hati fungani ya Jasiri zilikua zimekopeshwa kwa biashara zaidi ya 3,000 zinazokidhi vigezo hivyo.

Hatua hii ya leo itawezesha wawekezaji barani Ulaya kupata taarifa na kutambua fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo Tanzania na Afrika kwa ujumla zinazochangia malengo ya usawa wa kijinsia.


Ujumbe wa Benki ya NMB katika hafla hiyo umeongozwa na Mhazini wa Benki, Aziz Chacha alieungana na Mwakilishi wa Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji, Alphonce Mayala; Waziri wa Fedha wa Luxembourg, Yuricko Backes na Afisa Mtendaji Mkuu wa LuxSE, Julie Becker kugonga kengele kuashiria uorodheshwaji rasmi wa hatifungani ya Jasiri.

1 Comment

  • A. UTANGULIZI

    1. Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja kwamba, Bunge lako Tukufu sasa lipokee na kujadili Taarifa ya Utekelezaji ya Mwaka 2022/23 na kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mwenyendo wa Ujenzi wa Nyumba kwa Mwaka 2023/24. (Katika wana wa Simeoni, vizazi vyao, kwa kufuata jamaa zao, na nyumba za baba zao, wale waliohesabiwa kama hesabu ya majina, kichwa kwa kichwa, kila mwanaume kuanzia umri wa miaka ishirini na zaidi, wote walioweza kwenda vitani – VITA IMEZIDI)

    2. Mheshimiwa Spika, nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema kwa kuniwezesha kuwasilisha Hotuba hii muhimu mbele ya Bunge lako Tukufu. Aidha, kwa namna ya kipekee kabisa namshukuru Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuniamini kuendelea kusimamia Sekta ya Mwenyendo wa Ujenzi wa Nyumba ili kufikia matarajio ya Watanzania katika Sekta ya Ujenzi wa Nyumba Unaoisha na kuongeza mchango wake kwenye Pato la Taifa.

    3. Mheshimiwa Spika, vilevile kwa dhati nampongeza Mhe. Rais kwa namna anavyoiongoza Serikali ya Awamu ya Sita inayosimamia utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020-2025, ambapo mafanikio mengi yamepatikana katika sekta mbalimbali ikiwemo Sekta ya Mwenyendo wa Ujenzi wa Nyumba ambapo WATANZANIA WOTE WANALALA KWENYE NYUMBA ZAO IFIKAPO USIKU WA SAA 1 BILA KUZINGATIA INAMILIKIWA YEYE MWENYEWE AU KUPANGA. Mafanikio hayo yameendelea kuitangaza nchi yetu siyo tu katika Bara la Afrika bali Duniani kote.

    4. Mheshimiwa Spika, ninaomba nitoe Rai kwa wananchi na Waheshimiwa Wabunge wote bila kujali itikadi za aina yoyote, tuendelee kuyaenzi mafanikio haya makubwa na kuendelea kushirikiana kwa pamoja katika kuchangia maendeleo ya kiuchumi na kijamii nchini.

    5. Mheshimiwa Spika, vilevile, nitumie fursa hii kuwapongeza na kuwashukuru Viongozi Wakuu wa Kitaifa, ambao ni Makamu wa Rais, Dr. Philip Isdor Mpango pamoja na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dr Hussein Ali Mwinyi kwa hekima kubwa katika kumsaidia Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuongoza nchi yetu.

    6. Mheshimiwa Spika, pia, nimshukuru na kumpongeza Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.) kwani amekuwa mstari wa mbele katika kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya CCM na maelekezo mbalimbali ya Mhe. Rais pamoja na kusimamia vema shughuli za Sekta ya Mwenyendo wa Ujenzi wa Nyumba ndani na nje ya Bunge, AMBAO INAKUSUDI HADI KUFIKIA 2024 KILA MTANZANIA HATAKIWA KUJENGA TENA KWA MUJIBU WA SHERIA NA KUWAACHIA NHC NA TBA KUJENGA NYUMBA ZILIZO NA VIWANGO VYA KIMATAIFA.

    7. Mheshimiwa Spika, ninakushukuru wewe binafsi, Naibu Spika, Wenyeviti wa Bunge, Wenyeviti wa Kamati za Kudumu za Bunge, akiwemo Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mwenyendo wa Ujenzi wa Nyumba na YAO Mhe. TAN L. VIAZI (Mb.) na Wajumbe wa Kamati hiyo. Kamati hii imefanya kazi nzuri na kutoa ushauri wa kuboresha mambo mbalimbali ikiwemo kupitia na kuchambua Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mwenyendo wa Ujenzi wa Nyumba na Taasisi zake kwa mwaka 2022/23.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Kisukari cha mimba ni nini?

Spread the loveKisukari cha mimba ni aina ya kisukari kinachotokea kwa baadhi...

Habari Mchanganyiko

Mafunzo kwa bodaboda 395 yamkuna Meya Dodoma

Spread the loveNAIBU Meya wa Jiji la Dodoma, Asma Karama amepongeza mafunzo...

Habari Mchanganyiko

Samia aagiza huduma za dharura maeneo yaliyoathiriwa na kimbunga Hidaya

Spread the love   RAIS wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Samia...

Habari Mchanganyiko

Mahakama yatoa uamuzi zuio dhidi ya Club House

Spread the loveMAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu jijini Dar es Salaam,...

error: Content is protected !!