Wednesday , 8 May 2024
Home Habari Mchanganyiko NMB ‘yawapiga msasa’ wanawake wa TUICO Morogoro
Habari Mchanganyiko

NMB ‘yawapiga msasa’ wanawake wa TUICO Morogoro

Spread the love

WANAWAKE wa Chama cha Wafanyakazi wa Viwanda, Biashara, Taasisi za Fedha, Huduma na Ushauri Tanzania (TUICO), wametakiwa kuvutiwa na mafanikio kitaifa na kimataifa ya Hati Fungani ya Jasiri ya Benki ya NMB ‘NMB Jasiri Bond,’ na kuyatumia kama chachu ya kuendelea kuwa wateja waaminifu wa benki hiyo ili kuwa sehemu ya mnyororo wa wanufaika wa huduma zenye lengo la kusaidia ustawi wao kimaisha na kukua kiuchumi. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Idara ya Rasilimali Watu wa Benki ya NMB, Joanitha Mrengo, alipomwakilisha Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Ruth Zaipuna, katika Semina ya Kuwajengea Uwezo Wafanyakazi Wanawake ambao ni Wanachama wa Tuico Mkoa wa Morogoro, iliyofanyika kwa siku moja, ikihudhuriwa pia na viongozi wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) na Shirika la Kazi Duniani (ILO) na kudhaminiwa na benki hiyo.

Aprili mwaka jana, NMB ilihitimisha mauzo ya Hati Fungani ya Jasiri kwa kuvuna kiasi cha Sh. Bil. 74 na kuvuka lengo la kukusanya Shilingi bilioni 25 pesa zilizotumika kutanua wigo wa utoaji huduma za mikopo kwa kampuni zinazoendeshwa na wanawake, ama kampuni zinazozalisha bidhaa zinazowagusa wanawake nchini.

Ni mafanikio yaliyoipa NMB tuzo mbalimbali, zikiwemo za Hati Fungani Bora ya Mwaka iliyotolewa na Waandaaji wa Tuzo za Kimataifa za Mitaji kwa Wajasiriamali Wadogo na wa Kati kwa kushirikiana na Jukwaa la Ufadhili wa Ujasiriamali (SME’s Finance Forum), pamoja na Tuzo ya Platinum ya Kundi la Dhamana Endelevu iliyotolewa nchini Cambodia, kote ikitambulika kama hati fungani wezeshi kwa wanawake, kiasi cha kuorodheshwa kwenye Soko la Hisa la Luxemburg (LuxSE), ambalo ni moja ya masoko makubwa ya hisa duniani.

Akizungumza wakati akifungua semina hiyo, Mrengo alisema mafanikio hayo, pamoja na kutambuliwa kwa benki yake kuwa miongoni mwa taasisi kinara katika mgawanyo wa kiuchumi kwenye suala la kijinsia (EDGE Certificate), ambako NMB ni taasisi ya kwanza Afrika kutunukiwa cheti, vinapaswa kutazamwa kwa jicho la ziada na wanawake wote nchini, wanaopambania ukuaji wao kiuchumi.

Mkuu wa Idara ya Rasilimali watu wa Benki ya NMB,Joanitha Mrengo (kulia) akizungumza na Naibu Katibu Mkuu TUICO, Takim Salehe (kushoto) pamoja na mkurugenzi wa mashirika ya fedha TUICO, Peles Jonathan Hageze (katikati) baada ya kufungua Semina ya kuwajengea uwezo wafanyakazi wanawake wanachama wa TUICO Mkoa wa Morogoro.

“Wafanyakazi wanawake wanakabiliwa na changamoto nyingi katika maisha yao ya kazi, ikiwa ni pamoja na kutafuta Usawa wa Kijinsia, kujaribu kufikia malengo yao ya kazi na kuboresha Ustawi wa Jamii. Hivyo NMB tunaamini semina hii itawajengea uwezo katika nyanja za uongozi na uchumi.

“Sisi NMB tunatambua na kuthamini umuhimu wa kuendeleza na kuimarisha uwezo wa wanawake katika jamii yetu, kwani tunajua wanaweza kuchangia ukuaji wao kiuchumi na ustawi wa jamii inayowazunguka na taifa kwa ujumla, ndio maana tukatenga fungu kubwa la fedha za mikopo na huduma mbalimbali za kifedha kwa wanawake wajasiriamali na wafanyakazi,” alisisitiza Mermaid katika semina hiyo.

Mkuu wa Idara ya Rasilimali watu wa Benki ya NMB,Joanitha Mrengo akizungumza na kusalimiana na washiriki wa Semina ya kuwajengea uwezo wafanyakazi wanawake wanachama wa TUICO Mkoa wa Morogoro kutoka Sekta isiyo rasmi wa jamii ya Kimasai.

Naye Naibu Katibu  Mkuu wa TUICO, Tamim Salehe, aliishukuru NMB kwa kushirikiana na chama chake katika kuwanoa wanawake wanachama wa mkoa wa Morogoro, huku akiwataka washiriki wote kuitumia vema semina hiyo sio tu kwa kuzingatia maelekezo, bali pia kujenga mtandao wa kiushirikiano baina yao ili kusaidiana maarifa ya utatuzi wa changamoto mahali pa kazi ama biashara zao.

 

Tamim alizishukuru ATE, ILO, Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Wafanyakazi na taasisi nyingine kwa kushiriki na kufanikisha semina hiyo, ambayo pia ilitumika kuwaelimisha wanawake juu ya uongozi katika chama, jamii na taasisi za kazi, kuwaongezea uelewa wa agenda ya Usawa wa Kijinsia (50 kwa 50), kushirikisha wanawake katika shughuli na mipango ya TUICO – chama kinachojumuisha wadau wa sekta nne za Viwanda, Biashara, Taasisi za Fedha na Huduma na Ushauri.

2 Comments

  • NMB inafanya kufuru katika tozo zao
    Sisi wenye akanti tunakatwa fedha kibao eti za ATM card maintenance etc etc
    Hakuna benki hapa nchini inayotoza na kukata kama NMB
    Hivyo faida inayoonyesha NMB kila mwaka ni za WIZI

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC, SILABU waungana kufikisha elimu ya fedha majumbani

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeingia makubaliano ya ushirikiano...

AfyaHabari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Kisukari cha mimba ni nini?

Spread the loveKisukari cha mimba ni aina ya kisukari kinachotokea kwa baadhi...

Habari Mchanganyiko

Mafunzo kwa bodaboda 395 yamkuna Meya Dodoma

Spread the loveNAIBU Meya wa Jiji la Dodoma, Asma Karama amepongeza mafunzo...

Habari Mchanganyiko

Samia aagiza huduma za dharura maeneo yaliyoathiriwa na kimbunga Hidaya

Spread the love   RAIS wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Samia...

error: Content is protected !!