Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko NMB yatenga bilioni 20 mikopo kuchangia ukuaji sekta ya kilimo Tanzania
Habari Mchanganyiko

NMB yatenga bilioni 20 mikopo kuchangia ukuaji sekta ya kilimo Tanzania

Spread the love

BENKI ya NMB imetenga mikopo ya Sh20 bilioni itakayotumika kuchangia maendeleo ya sekta ya kilimo nchini ikiwa ni dhamira ya benki hiyo katika kuinua ufanisi wa sekta hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kushuhudia uzinduzi wa programu ya Serikali ya vijana maarufu kama ‘Building Better Tomorrow’ (BBT) Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma linalolenga kukuongeza ushiriki wa vijana wa Kitanzania katika kilimo biashara, Mkuu wa Wateja Wadogo wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi alisema juhudi za benki zinalenga kuunga mkono Ajenda ya 10/30 ya Serikali.

Mbunge wa Mchinga na mke wa Rais Mstaafu wa Awami ya nne, Salma Kikwete (katikati) akisalimiana na Afisa Mkuu wa wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi (Kulia) baada ya uzinduzi wa programu ya Mashamba makubwa (block farming). Benki ya NMB imeshiriki katika uzinduzi na tayari wametenga shilingi bilioni 20 kwaajili ya mikopo kwa ajili ya wanaoanza kujihusisha ni kilimo. Kushoto ni mkuu wa idara biashara za serikali wa Benki ya NMB, Vicky Bishubo

Uzinduzi huo ulifanywa na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan. 

Mponzi alibainisha jitihada za benki yake siyo tu zitasaidia katika kupanua shughuli za kiuchumi katika sekta ya kilimo bali pia zitasaidia kuongeza usalama wa chakula.

“Benki ya NMB ni mdau mkubwa sana wa serikali na tumekuwa tukishirikiana na sekta mbalimbali ikiwemo sekta hii ya Kilimo. Sekta hii ni muhimu sana kwa uchumi wa nchi yetu.

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe (katikati) akisalimiana na Afisa Mkuu wa wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi (Kulia) baada ya uzinduzi wa programu ya Mashamba makubwa (block farming). Benki ya NMB imeshiriki katika uzinduzi na tayari wametenga shilingi bilioni 20 kwaajili ya mikopo kwa ajili ya wanaoanza kujihusisha ni kilimo. Kushoto ni mkuu wa idara biashara za serikali wa Benki ya NMB, Vicky Bishubo

Benki yetu itaendelea kuwa bega kwa bega na wizara ya kilimo ili kuhakikisha maono yake katika sekta ya Kilimo hapa nchini yanatimia na kuzidi kukuza uchumi wa nchi yetu,” alisema

Mponzi alisema,”ni imani yetu kuwa juhudi zetu zitasaidia kujenga sekta ya kilimo imara yenye ushindani na jumuishi na yenye sifa ya kuimarika kwa ufanisi, utofauti na yenye kuongeza mapato.”

Mponzi alisema mara baada ya benki yake kushirikishwa na wizara ya kilimo juu ya mpango huo wa Building a Better Tomorrow, benki yake haikusita kuridhia kushirikiana na wizara na ilitoa wataalamu wake kudadavua vyema mkakati huo na badae kuanzisha huduma ambazo zitasaidia  ufanisi wa mkakati huu.

“Tumekuja na bidhaa ya mkopo maalum wenye riba rafiki ambao utawawezesha Vijana kupata mitaji ya kuanzisha au kuendeleza biashara za kilimo, ufugaji na uvujiwa. Maana tunatambua changamoto kubwa ya vijana wengi kuingia katika kilimo ni ukosefu wa mitaji, hivyo Benki ya NMB imeona kwa kuanzisha mkopo huu maalum basi wengi watashawishika na adhma ya Building a Better Tomorrow itatimia,” alisema Mponzi.

Aliwataka vijana kuchangamkia fursa hiyo kwa kutembelea matawi ya benki hiyo yaliyopo nchini kote huku akisema kuwa benki yake imetoa mafunzo ya kifedha kwa vijana zaidi ya 800 ambao wamechaguliwa kushiriki program ya BBT.

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe wakati wa uzinduzi wa programu ya BBT alisema tayari wizara yake imeshirikisha benki mbalimbali zinazofanya kazi nchini Tanzania kuanzisha fungo maalum yaani ‘matching fund’ ili kuunga mkono juhudi za wizara hiyo zinazolenga kufufua na kufungua sekta ya kilimo.

“Nina furaha kutangaza kwamba tayari nimeshapokea barua kutoka benki ya NMB na wametoa ahadi ya kutoa shilingi bilioni 20 ambazo zimetengwa na benki hiyo kusaidia mpango huu na tutaendelea kushirikiana na benki hiyo katika kutekeleza hili,” Bashe alisema.

Bashe alisema Serikali imejipanga kikamilifu kusaidia vijana katika mnyororo wa thamani wa sekta ya kilimo ili kuwasaidia kutimiza ndoto zao kikamilifu kupitia biashara ya kilimo.

“Kihistoria mashamba mengi ya vitalu yaliyoanzishwa yalikufa kwa sababu ya ukosefu usimamizi mzuri wa umiliki kwani mengi yalionekana kama mashirika ya umma na wale walioshiriki walifanya hivyo kwa burudani na sio biashara. 

 Tunaposonga mbele sasa, mashamba yote ya vitalu lazima yawe na umiliki na hii itasaidia katika uwajibikaji,” Bashe alisema.

Kuhusu dhamira ya Serikali ya kuongeza thamani ya korosho ya Tanzania, Bashe alibainisha kuwa kuanzia bajeti ya mwaka wa fedha wa 2026/2027, korosho za haitauzwa kama mali ghafi.

 ““Tayari tumefanya mradi wa majaribio na hadi sasa tumefanikiwa kupata hekta 1000 katika wilaya ya Nanyamba ambapo tutajenga kiwanda cha kusindika tani 300,000. Juhudi zetu zitahakikisha uongezaji thamani wa korosho zetu.

 Inasikitisha kwamba baadhi ya watu hawajishughulishi na shughuli za kila siku za sekta ya kilimo lakini wanafanya maamuzi kwa niaba ya wakulima,” Bashe alisema.

Lengo la serikali ni kufikia ukuaji wa zaidi ya asilimia 10 kwa sekta ya kilimo ifikapo 2030

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

error: Content is protected !!