Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Dk. Tax, balozi wa Marekani wajadili mapokezi ya Kamala Harris
Habari Mchanganyiko

Dk. Tax, balozi wa Marekani wajadili mapokezi ya Kamala Harris

Spread the love

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Stergomena Tax amekutana na kuzungumza na Balozi wa Marekani nchini, Michael Battle katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Pamoja na mambo mengine, viongozi hao wamejadili kuhusu maandalizi ya ziara ya Makamu wa Rais wa Marekani nchini, Kamala Harris, masuala ya ushirikiano kati ya Tanzania na Marekani na jinsi ya kufanya kazi kwa pamoja katika kuendeleza uhusiano wa kidiplomasia uliopo baina ya mataifa hayo mawili.

Dk. Tax ameishukuru Serikali ya Marekani kwa kushirikiano na Serikali ya Tanzania wakati wote tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya mataifa hayo na umekuwa na maslahi mapana kwa wananchi wa pande zote mbili.

Naye Balozi wa Marekani Nchini, Battle ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuendelea kudumisha uhusiano wake na Serikali ya Marekani.

Katika tukio lingine, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk amekutana kwa mazungumzo na Balozi wa Urusi nchini, Andrey Avetisyan katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Balozi Mbarouk ameipongeza Urusi kwa fursa za masomo zinazotolewa na nchi hiyo kwa watanzania na kuomba fursa zaidi za ushirikiano katika sekta za kilimo, madini, afya na uhandisi.

Naye Balozi wa Urusi, Andrey Avetisyan amesema Serikali ya Urusi inategemea kuongeza idadi ya ufadhili wa nafasi za masomo kutoka idadi ya nafasi 90 hadi 120 ili kutoa nafadi zaidi kwa watanzania kunufaika na fursa za elimu zinazopatikana nchini Urusi.

Urusi imekuwa ikishirikiana na Tanzania katika nyanja mbalimbali hususan sekta za elimu, afya, utalii na utamaduni, mafuta na gesi, ulinzi na usalama, madini, kilimo na uhandisi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

error: Content is protected !!