Wednesday , 1 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa NEC yamteua Magufuli kugombea urais Tanzania
Habari za Siasa

NEC yamteua Magufuli kugombea urais Tanzania

Spread the love

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imemteua Rais John Magufuli kuwa Mgombea Urais wa Tanzania na Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea mwenza, kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Wagombea hao wa CCM wameteuliwa leo Jumanne tarehe 25 Agosti 2020 baada ya kurudisha fomu za uteuzi za NEC sambamba na kukidhi masharti ya kikatiba.

Akitangaza uteuzi huo, Jaji Semistocle Kaijage, Mwenyekiti wa NEC amesema, tume hiyo imewateua baada ya kujiridhisha wamekidhi matakwa ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“NEC baada ya kujiridhisha wagombea waliopendekezwa na CCM wametimiza masharti ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na kwa mamlaka niliyopewa chini ya kanuni ya uchaguzi wa Rais na Wabunge tume imewateua Dk. Magufuli kuwa mgomeba kiti cha urais wa Tanzania na Samia kuwa mgombea wa kiti cha makamo wa urais Tanzania,” amesema Dk. Kaijage.

Dk. Willson Mahera, Mkurugenzi wa Uchaguzi NEC ametaja vigezo ambavyo vimepelekea wagombea hao kuteuliwa na NEC kugombea Kiti cha Urais wa Tanzania katika uchaguzi huo.

Mwenyekiti wa NEC, Semistocles Kaijage

“Wagomeba kiti cha rais na makamo wa rais wa CCM Dk. Magufuli wametimiza masharti ya uteuzi kama ifuatavyo, moja fomu ya uteuzi zimejazwa kwa ukamilifu inavyotakiwa, wametoa tamko la kuwa wanazo sifa za kugomeba, “ amesema Dk. Mahera.

Dk. Mahera amesema, “Katibu Mkuu wa chama ametoa uthibitisho wa kugombea, wamedhaminiwa na wadhamini wa mikoa 10 na mitano ya ziada. Wasimamizi wa uchaguzi wamethibitisha majina ya udhamini.”

Dk. Mahera amesema wagombea hao wa CCM pia wametimiza masharti ya kutoa tamko mbele ya Jaji wa Mahakama Kuu kuwa wana sifa za kuteuliwa pamoja na kuwasilisha NEC nakala nne za sifa za kila mgombea.

Akizungumza wakati anakabidhi fomu hizo , Rais Magufuli amesema amepata wadhamini katika mikoa 15.

“Kama nilivyosema tuna wadhamini katika mikoa 10 lakini pia na katika mikoa mitano jumla mikoa 15,” amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli na Mama Samia walisindikizwa na Dk. Bashiru Ally, Katibu Mkuu wa CCM pamoja na Humphrey Polepole, Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM.

Zoezi la uchukuaji na urudishaji fomu lilianza tarehe 5 Agosti 2020 na kukamilika leo tarehe 25 Agosti 2020, ambapo pia ni siku ya uteuzi wa wagombea.

Rais Magufuli na mgombea wake mwenza walichukua fomu hizo tarehe 6 Agosti 2020 siku moja baada ya zoezi hilo kufunguliwa na NEC.

CCM kinatarajia kuzindua kampeni zake tarehe 29 Agosti 2020 jijini Dodoma, siku hiyo hiyo ambapo chama hicho kitazindua ilani yake ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

error: Content is protected !!