Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Tundu Lissu aibua hofu mpya
Habari za Siasa

Tundu Lissu aibua hofu mpya

Tundu Lissu-Chadema
Spread the love

HOFU mpya imeanza kutanda nchini Tanzania juu ya hatma ya mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano, kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu, kufuatia madai kuwa aweza kuenguliwa kugombea nafasi hiyo. Anaripoti Saed Kubenea…(endelea).

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya Chadema, hofu ya kuenguliwa kwa Lissu inatokana na kuzagaa mitandaoni, kwa madai kuwa kuna mpango wa kumuengua mwanasiasa huyo, kwa kutumia sababu mbalimbali za kisheria, ikiwamo makosa ya kimaadili na kuanza kampeni mapema.

Hata hivyo, Lissu mwenyewe, amewahi kujibu madai hayo mara kwa mara akisema, anachofanya sio kuanza kampeni kabla ya wakati, na kwamba hakuna sheria yeyote inayozua mtu kuanza kampeni kabla ya muda uliowekwa.

Alisema, akiwekewa pingamizi naye ataweka dhidi ya mgombea urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais John Magufuli kwa madai kuwa amekuwa akifanya kampeni kwa miaka yote mitano.

Kama hiyo haitoshi, Lissu alidai kuwa hivi karibuni Rais Magufuli baada ya kuteuliwa na chama chake kuwa mgombea urais, alitoa fedha zaidi ya Sh. 100 milioni na Sh. 100,000 kwa mwananchi aliyemzawadia kuku, jambo ambalo alidai ni sawa na rushwa.

Mwenyekiti wa NEC, Semistocles Kaijage

Madai ya kuwapo mkakati wa kutaka kuliengua jina la Lissu, kwa mara ya kwanza juzi yamemuibua mwenyekiti wa chama chake taifa, Freeman Mbowe.

Akiandika katika ukurasa wake wa twitter, Mbowe alisema, “hakuna uchaguzi kama jina la Lissu halitakuwapo kwenye kinyang’anyiro hicho.”

Alisema, “Watanzania wenzangu, tuna masaa 24 (saa 24), kwa NEC kuweka Misingi ya Amani ya Tanzania. Mkakati wowote wa kuengua kwa hila wagombea wetu, utapokelewa kwa kishindo kikubwa. #NoLissuNoElection!SasaBasi. Uzalendo uonyeshwe kwa kusimamia haki na si vinginevyo.”

Tume ya taifa ya uchaguzi (NEC), inatarajiwa kufanya uteuzi kwa wagombea urais wa vyama vyote vinavyosumamisha wagombea wake.

Mbali ya Lissu, hofu ya kuenguliwa kwa wagombea ubunge na udiwani, nayo imetanda karibu nchi mzima. Hofu ya safari hii, inatokana na historia ya kilichotokea kwenye chaguzi ndogo za ubunge na uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji.

Katika baadhi ya maeneo, tayari kumepatikana malalamiko kuwapo kwa madai ya kunyimwa fomu kwa baadhi ya wagombea wateule wa Chadema katika majimbo ya Kilombero mkoani Morogoro, Kigamboni, Kibamba na Mbagala jijini Dar es Salaam.

4 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Dk. Mwakyembe : Zanzibar waliongoza kutaka Serikali 2 za muungano

Spread the love  MWANASIASA mkongwe nchini, Dk. Harrison Mwakyembe, amesema mjadala wa...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataja mikakati ya kufikia trilioni 2 biashara Uturuki, Tz

Spread the loveWakati Tanzania na Uturuki zikidhamiria kuongeza kiwango cha biashara hadi...

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

error: Content is protected !!