Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Ndaruke achanguliwa Mwenyekiti mpya CCM Kibiti
Habari za Siasa

Ndaruke achanguliwa Mwenyekiti mpya CCM Kibiti

Mshindi wa pili kwenye uchanguzi wa ndani wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kibiti kwenye nafasi ya Mwenyekiti Abdujabiri Malombwa (kushoto) akimpongeza mshindi wa uchanguzi huo Juma Kassim Ndaruke baada ya kutangazwa mshindi wa nafasi hio kwenye uchanguzi huo ambao ulifanyika Jumapili tarehe 2 Oktoba 2022.
Spread the love

 

Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Kibiti mkoani Pwani kimepata viogozi wapya baada ya kufanyika uchanguzi wa ndani wa chama hicho hapo jana, Jumapili tarehe 2 Oktoba 2022, ambapo Juma Kassim Ndaruke ameibuka kidedea baada ya kumshinda mpinzani wake wa karibu Abdujabiri Malombwa ambaye alikuwa akitetea nafasi hiyo kwa mara ya tatu.

Katika nafasi hiyo ambayo wagombea walikuwa watatu, Ndaruke alishinda kwa kupata kura 428 dhidi ya 385 za Malombwa huku mgombea wa tatu Abdallah Mpili akipata kura 7.

Kuchanguliwa kwa Ndaruke kuna maanisha kuwa ndio atakuwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kibiti kwa miaka mitano ijayo (2022-2027).

Akizungumza na Wajumbe wa Mkutano wa chama hicho ngazi ya wilaya ambao ndio walikuwa wapiga kura, Ndaruke alisema kuwa ni fahari kuona wajumbe wakiwapa nafasi za uongozi vijana ndani ya chama.

“Hii inaonyesha ni kwa kiasi ngani CCM ilivyo wekeza kwenye kukuza vijana. Nachukua fursa hii kwanza kumshukuru Mungu, wajumbe pamoja na kila mmoja wetu aliyeshiriki kwenye uchanguzi. Naomba kusema kuwa hapa aliyeshinda sio Ndaruke mbali CCM ndio imeshinda.

“Tunapokwenda kuanza kazi na uongozi upya nataka kukuchukua fursa hii niwaambie kuwa tutaenda kujenga CCM imara yenye dira na ambayo itakuwa na uwezo wa kuisimamia serikali ili kuhakikisha ya kwamba miradi ya maendeleao kwenye wilaya yetu inatekelezwa pamoja na kumalizika kwa wakati,” alisema Ndaruke ambaye pia ni Mwenyekiti wa UVCCM mstaafu wa wilaya hiyo’.

Akizungumza baada ya kukubali matokeo, mpinzani wa karibu wa Ndaruke na ambaye pia alikuwa anatetea nafasi hiyo Malombwa alisema “Nachukua fursa hii kumshukuru Mwenyekiti wetu mpya na kusema kuwa nimekubali ya kuwa nimeshindwa kihalali kabisa. Lazima tukubali kuwa uongozi ni kupokezana vijiti, muda wangu wa utumishi kama Mwenyekiti wa wilaya umemalizika na kwa sasa kijiti namuachia Ndugu Ndaruke’.

Kwenye uchaguzi huo, kulikuwepo na nafasi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Mkoa ambao walioshinda ni Ashura Matimwa na Uwesu Mtandika na nafasi Mkutano Mkuu Taifa ambao walioshinda ni Ally Seif, Khalid Mtalazaki na Rehema Mkumba.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

error: Content is protected !!