Friday , 17 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Waziri wa Madini aridhishwa kasi ya ujenzi wa kinu cha kupoza umeme GGML
Habari Mchanganyiko

Waziri wa Madini aridhishwa kasi ya ujenzi wa kinu cha kupoza umeme GGML

Spread the love

WAZIRI wa Madini Dk. Dotto Biteko ameeleza kuridhishwa na kasi ya ujenzi wa kinu cha kupoza umeme (substation) kinachojengwa na Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) ili kuwezesha mgodi huo kuachana na uzalishaji wa umeme wa mafuta na kuhamia kwenye umeme wa Gridi ya Taifa ambao ni nafuu zaidi. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Mgodi huo wa GGML unajenga kinu hicho kitakachokuwa na uwezo wa kupitisha umeme wenye kilovolt 13 kwenye mitambo yake ambapo hadi kikamilike kinatarajiwa kugharimu kiasi cha Sh bilioni 50.

 

Waziri wa Madini, Dk. Dotto Biteko (wa pili kulia) akipatiwa maelezo kuhusu mradi wa kinu cha kupoza umeme kutoka kwa Meneja anayehusika na miundombinu kutoka GGML, Eliakimu Kagimbo. Dk. Biteko alitembelea mgodi wa GGML pamoja na mradi huo unaojengwa na kampuni hiyo ili kupokea umeme wa Tanesco na kuuwezesha mgodi kuanza kutumia umeme wa Gridi ya Taifa badala ya umeme unaozalishwa kwa mafuta ya dizeli.

Aidha, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) nalo linajenga njia ya kupeleka umeme katika mgodi wa GGML yenye urefu wa kilomita sita.

Hayo yamebainishwa katika ziara ya Waziri wa Madini aliyoifanya juzi katika Mgodi wa GGML uliopo Geita ambapo pamoja na mambo mengine alisema anaamini hadi kufikia Machi mwaka 2023, GGML itaanza kutumia umeme wa gridi ya Taifa.

“GGML wanataka kuhama kutoka kwenye matumizi ya umeme unaozalishwa kwa mafuta kwenda kwenye umeme wa TANESCO, kupitia substation inayojengwa kwa dola za Kimarekani milioni 20, na wamekwenda kwenye hatua nzuri, naamini mpaka itakapofika Machi mwaka kesho tutawasha umeme wa TANESCO kuendesha mgodi wetu hapa ndani,” amesema Dkt. Biteko.

Awali, Makamu Rais wa kampuni ya AngloGold Ashanti inayomiliki Geita Gold Mining Limited (GGML), Simon Shayo amesema kukamilika kwa mradi huo kutapunguza gharama za uendeshaji wa mgodi na uzalishaji wa umeme kwa asilimia zaidi ya 50.

Alisema mgodi wa GGML unatumia zaidi ya MW 40 zinazozalishwa kwa kutumia jenereta zinazotumia mafuta ya dizeli tangu mwaka 2018.

“Sasa tupo kwenye mchakato wa kujenga kinu cha kupoozea umeme chenye thamani ya karibu Shilingi za Kitanzania bilioni 50 na TANESCO watajenga njia ya kilomita sita kufikia hapa.

“Kwa hiyo hadi kufikia Machi mwaka 2023, tutakuwa tumeingia kwenye umeme wa TANESCO, na tutakuwa tumepunguza gharama yetu ya umeme kufikia asilimia 50, kutoka uniti moja kwa senti 19 kwenda kwenye unit moja kwa senti tisa (US $),” alisema.

Aidha, ilielezwa kuwa kukamilika kwa mradi huo wa kupeleka umeme kwenye Kampuni ya GGML kunatarajiwa kutaliwezesha Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kupata shilingi bilioni tano za kitanzania kwa mwezi zitakazotokana na mauzo ya umeme.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Udhibiti wa serikali wakera asasi za kiraia

Spread the loveBaadhi ya wadau wa demokrasia na viongozi wa asasi za...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Nape aomba bajeti ‘kiduchu’ kwa mwaka 2024/25

Spread the loveWaziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Seneta: Wanasiasa hawasaidii mchakato wa Katiba mpya

Spread the loveSeneta wa jimbo la Busia, nchini Kenya, Okiya Okoiti Andrew...

Habari Mchanganyiko

Wananchi washauriwa kuongeza uelewa wa kujikinga na majanga

Spread the love WITO umetolewa kwa wananchi kuongeza uelewa na utayari kabla...

error: Content is protected !!