November 30, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia: Linaloamuliwa na Serikali ni lako Waziri

Rais Samia Suluhu Hassan

Spread the love

RAIS Samia Suluhu Hassan amewapa maelekezo mawaziri ikiwemo kutunza siri na kubeba jambo lolote linaloamuliwa na Serikali. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Mkuu huyo wa nchi amesisitiza kuwa Waziri hawezi kujitenga na uamuzi wowote wa Serikali na anapaswa kujua namna ya kutumia siri katika kufanya kazi zake.

Rais Samia ameyasema hayo leo Jumatatu tarehe 3 Septemba, 2022, mara baada ya kuwaapisha Mawaziri wapya watatu Ikulu jijini Dar es Salaam. Mawaziri walioapishwa ni pamoja na Innocent Bashungwa,

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa; Stergomena Tax, Waziri wa Mambo ya Nje na Jumuiya ya Afrika Mashariki na Angela Kairuki Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.

“Linaloamuliwa na Serikali Waziri ni lako, unatakiwa ulibebe na kulifanyia kazi kwa misingi ile uliyoelekezwa, huwezi kusema nimeelekezwa hivi lakini mimi sikutaka hivi nafanya kwasababu nimeelekezwa, huwezi kujitoa,” amesema Samia.

Mbali na hilo Rais Samia amewataka mawaziri kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo wameapa kwayo.

“Katika viapa vyenu mnaapa kuitetea na kuilinda katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania… kwahiyo ni muungano wenye pande mbili na mtatumika kwa pande zote sawa kwa jinsi Katiba ilivyogawa mipaka,” amesema.

Jambo lingine awetaka kujua mipaka ya kazi zao na pindi wanapotaka kuvuka mipaka hiyo kuomba ruhusa.

“Nchi hii ina mamlaka na mamlaka uliyowekewa ina mipaka yake, unapotaka kuvuka lazima kupata ruhusa kutoka kwa mamlaka ya juu kwahiyo unatakiwa kujua ukomo wa mamlaka kwenda juu na kushuka chini,” amesema.

Rais Samia amesema mambo hayo matatu ndiyo msingi wa kufanya kazi zao na kwamba mambo mengine ya ksekta atawaelekeza mmoja mmoja.

error: Content is protected !!