Monday , 11 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Mwenyekiti CCM Arusha afariki dunia, Chongolo, Silaa wamlilia
Habari za SiasaTangulizi

Mwenyekiti CCM Arusha afariki dunia, Chongolo, Silaa wamlilia

Zelote Stephen
Spread the love

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Arusha, Zelote Stephen amefariki dunia jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Katibu wa CCM mkoa Arusha, Mussa Matoroka amesema wamepata taarifa za kifo hicho leo jioni Alhamis tarehe 26 Oktoba 2023.

“Ni kweli Mwenyekiti amefariki jijini Dar es Salaam ambapo alikuwa amekwenda kupatiwa matibabu…huu ni msiba mkubwa kwetu CCM, familia ndugu na jamii,” amesema Matoroka.

Pia kwa mujibu wa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa amendika katika akauti yake ya mtandao wa Instagram kuhusu taarifa za kifo cha kada huyo wa CCM na kuongeza kuwa mipango ya maazishi inafanywa nyumbani kwake Seaview Upanga jijini Dar es Salaam.

“Maziko yatafanyika nyumbani kwake Olasiti Arusha kwa tarehe itayotangazwa. Kwa kuwa ni ngumu kumtaarifu kila mmoja, naomba mpokee taarifa hii kwa wote. Tumwombee marehemu na tuiombee familia katika kipindi hiki cha msiba,” ameandika Silaa.

Aidha, katika ukurasa wake wa Instagram, Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo ameweka picha ya Marehemu Stephen huku akiandika maneno yanayoonyesha kuumizwa na kifo hicho.

“Taarifa za kuondokewa na Zelote Stephen, Mwenyekiti wetu wa CCM mkoa wa Arusha ni taarifa za kusikitisha sana. Kwani kwa hakika kifo chake kimetunyima fursa muhimu ya kuendelea kujifunza mengi na kuuishi uongozi wake”

“Mungu ameendelea kutufunza. Mipango yetu imekwama. Nenda Laigwanan. Nenda mzee wangu. Nilipokutembelea siku chache zilizopita hospitali ulinipa matumaini. Kumbe mipango ya Mungu ikabaki. Wewe ni shujaa, Nenda Kamanda”, imesomeka sehemu ya taarifa hiyo.

Stephen kabla ya kuwa Mwenyekiti wa CCM mkoani Arusha, pia aliwahi kutumia nafasi mbalimbali ndani ya Serikali hususani Jeshi la Polisi ambako alikuwa Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma na Rukwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Biteko: Samia ni muumini wa maridhiano sio kwa kuigiza

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Mpango: Sitakufa bali nitaishi

Spread the loveMAKAMU  wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk....

Habari za SiasaTangulizi

Mbowe: Miaka 62 ya uhuru tujenge upya mioyo yetu

Spread the loveWAKATI Tanganyika ikiadhimisha miaka 62 tangu kupata uhuru, Mwenyekiti wa...

Habari za Siasa

Rais Samia asamehe wafungwa 2,244

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewasamehe wafungwa 2,244, huku akiwabadilishia...

error: Content is protected !!