Friday , 1 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Mchango wa wachimbaji wadogo wafikia  asilimia 40 
Habari Mchanganyiko

Mchango wa wachimbaji wadogo wafikia  asilimia 40 

Spread the love

WAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde amesema kutoka na serikali kuweka mazingira mazuri kwenye sekta ya madini, mchango wa wachimbaji wadogo umeweza kufikia asilimia 40. Anaripoti Selemani Msuya …(endelea).

Mavunde amesema hayo jana wakati akimkaribisha Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kufunga Jukwaa la Uwekezaji wa Madini Tanzania linalofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 25 hadi 26, 2023.

Amesema wachimbaji wadogo wamekuwa wakiongezeka siku hadi siku hali ambayo inachangia mchango wao kwenye pato la taifa kuongezeka pia.

“Mheshimiwa Waziri Mkuu, sekta ya madini imeendelea kukuwa na kwa sasa mapato ya sekta hiyo ni zaidi ya dola milioni 678, na asilimia 40 ya mchango huo unatoka kwa wachimbaji wadogo,”amesema.

Amesema wizara hiyo imejipanga kutekeleza maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa ufanisi mkubwa ili sekta hiyo iweze kuwa na mchango mkubwa kwenye pato la Taifa na kuchochea maendeleo.

Kwa upande mwingine Waziri  Mavunde amesema sekta hiyo inaenda kukua zaidi ambapo kwa mara ya kwanza Tanzania imeanza kuchimba madini ya  Hellium huko mkoani Rukwa.

Mavunde amesema watahakikisha wanatumia fursa ya uwepo wa madini mkakati ambayo yamekuwa adimu na kuhitajika duniani kote, kuchangia maendeleo.

Amesema mkutano huo umekua wa mafanikio makubwa wamejifunza na kupata fursa za uwekezaji na miradi ya madini mkakati na mengine.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Karafuu, Parachichi yawa fursa Morogoro

Spread the loveIMEELEZWA kuwa zao la karafuu ambalo kwa sasa linalimwa pia...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Washindi 12 NMB MastaBata na wenza wao wapaa Afrika Kusini

Spread the loveWASHINDI 12 wa kampeni ya kuhamasisha matumizi yasiyohusisha pesa taslimu...

Habari Mchanganyiko

4 wanusurika kifo ajali ya ndege Serengeti

Spread the loveWATU wanne wakiwamo abiria watatu na rubani mmoja wamenusurika kifo...

Habari Mchanganyiko

Mafua yamtesa Papa, afuta mikutano

Spread the loveKiongozi wa Kanisa katoliki duniani, Papa Francis amelazimika kufuta mkutano...

error: Content is protected !!