Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Tangulizi Mwanaye Rais Museveni atangaza kustaafu jeshi Uganda
Tangulizi

Mwanaye Rais Museveni atangaza kustaafu jeshi Uganda

Spread the love

KAMANDA wa jeshi la ardhini nchini Uganda (UPDF), Luteni Jenerali Muhoozi Kainerugaba ametangaza kustaafu katika jeshi hilo baada ya kuhudumu kwa miaka 28. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Hata hivyo, ombi lake la kutaka kustaafu linatarajiwa kuidhinishwa chini ya kifungu cha sheria za jeshi la UPDF 2005.

Aliandiaka katika ujumbe wake wa twitter: “Baada ya kuhudumu kwa miaka 28 katika jeshi letu, jeshi bora zaidi duniani, nafurahia kutangaza kwamba ninastaafu.

“Mimi na wanajeshi wangu tumefanikiwa pakubwa, ninawapenda na kuwaheshimu maafisa wote waliofanikiwa kila siku,” alisema mtoto huyo wa Rais wa Uganda Yoweri Museveni katika mtandao wake wa twitter.

Muhoozi ambaye alipanda ngazi katika jeshi hilo alisema kwamba yeye na wanajeshi wake wamepata mafanikio makubwa.

Kwa mujibu wa gazeti la The Monitor nchini Uganda, tayari huduma za mitandao ya kijamii ikiwemo Twitter na facebook zimetawaliwa na jumbe za Muhoozi kuwa rais mtarajiwa wa Uganda licha ya Muhoozi mwenye umri wa miaka 47 kukataa kutangaza hadharani.

Tayari ujumbe huo umechukuliwa na kuwekwa katika akaunti ya twitter ya jeshi la UPDF.

Kwa mujibu wa sheria za jeshi, afisa anaweza kuwasilisha ombi la kustaafu katika bodi lakini hawezi kuondoka jeshini hadi pale ombi lake litakapoidhinishwa na bodi ya jeshi kulingana na kifungu 66(1) .

Nchini Uganda, maofisa wakuu wa jeshi akiwemo jasusi wa zamani wa taifa hilo Jenerali David Sejusa, awali alikataliwa ombi lake la kutaka kustaafu ama hata kucheleweshwa kulingana na gazeti la The Monitor Uganda.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kwafukuta kisa chaguzi, Lissu aibua tuhuma nzito

Spread the loveCHAGUZI za kusaka viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo...

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga “HIDAYA” chaendelea kuimarika, wananchi wapewa tahadhari

Spread the loveMAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inaendelea kutoa taarifa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali yaanza msako wanaotoa mikopo kausha damu

Spread the loveSERIKALI imeanza kufuatilia watu, vikundi na taasisi zinazotoa kinyume cha...

error: Content is protected !!