October 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Video za mahojiano mke wa msuya, polisi zakwama kortini, Jaji kutoa uamuzi

Spread the love

 

UPANDE wa utetezi kwenye kesi inayomkabili, mke wa bilionea Msuya, Miriam Mrita na mfanyabiashara Revocatus Muyella umepinga kilelezo chenye ushihdi wa video iliyodaiwa kurekodiwa wakati wa mahojiano ya mtuhumiwa huyo na polisi. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Kwenye shauri hilo, Mrita na Muyella wanadaiwa kumuua kwa kumchinja dada wa marehemu Msuya, Aneth Msuya nyumbani kwake Kigamboni jijini Dar es Salaam tahere 25 Mei 2016 ikidaiwa Allan Kimario (4) akishuhudia .

Leo tarehe 8 Machi, 2022 mbele ya Jaji Edwin Kakolaki kwenye Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, upande wa Jamhuri ukiwasilisha ushahidi wao uliobebwa na shahidi wa sita Inspekta Alistides Kasigwa ambaye ni mchunguzi wa picha mbalimbali zinazohusu matukio ya kihalifu na zile zisizokuwa na kihalifu.

Kasigwa akiongozwa na wakili mwandamizi wa wa serikali, Genes Tesha huku upande wa utetezi ukiwakilishwa na Wakili Peter Kibala aliyesaidiwa na Nehemia Nkoko.

Tesha alimuongoza shahidi huyo kuanza kutoa ushahidi wake kwenye Mahakama hiyo na kwamba ushahidi wake ulibebwa na vielelezo viwili kimoja bahasha na cha pili ni tape aliyodai ndiyo iliyotumika kurekodi mahojiano yake na Ofisa wa Polisi kutoka kwenye Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaa SP Latifa Mohamed (42).

Inspekta Kasigwa alidai mahakamani hapo kuwa tarehe 8 Agosti 2016 alipewa jukumu la kurekodi video ya mahojiano hayo na kwamba alitumia kamera yake aliyoitaja aina ya Sony , betri, tape za min-div , chaja ya kamera na standi yake.

Akieleza mahakamani hapo aliamuriwa kwenda kituo cha Polisi cha uwanja wa ndege jijini Dar es Salaam, ambapo aliwakuta askari David Mhang’aya Jumanne Malaghahe na baadaye aliingia kwenye chumba cha mahojiano alimkuta mtuhumiwa wa kike pamoja na SP Latifa ndipo wakaanza mahojiano hayo huku yeye alikuwa akirekodi kupitia kamera yake na kwamba alidai kuwa alitumia dakika 40 kurekodi mahojiano hayo.

Alipoulizwa kwa huyu mtuhumiwa akimuona atamjua akadai kuwa atamfahamu na kwamba hapo mahakamani yupo ndipo akaamriwa na wakili Tesha akamuoneshe ndipo alipokwenda upande wa washtakiwa na kuonesha kwa kunyoosha mkono wake wa kushoto upande alioketi Mrita.

Inspekta Kasigwa alidai katika mahojiano hayo mtuhumiwa huyo alieleza angeweza kwenda nao Kibada-Kigamboni kuwaonesha eneo la tukio na kwamba walikwenda mpaka Kigamboni ambapo huko alirekodi mahojiano hayo yaliyotumia takribani dakika 10 mpaka 15.

Baada ya kumaliza mahojiano hayo Kasigwa alirejea Ofisini kwake na kuandaa Nakala mbili kwenye DVD, na tape moja akadai kuwa alizifunga k vizuri kishwa kuweka saini yake juu ya bahasha.

Inspekta Kasigwa aliiomnba mahakama hiyo kupokea bahasha hiyo kama kielelezo Jaji Kakolaki alipokea bahasha baadaye Wakili Tesha aliomba mahakama hiyo imrejeshee tena bahasha hiyo ambapo alirejeshewa na kumtaka Shahidi huyo aifungue na aeleze kilichopo ndani ya bahasha hiyo.

Shahidi huyo alifungua bahasha hiyo na kutoa tape ambayo alidai kuwa ndiyo aliyoitumia kurekodi mahojiano ya Mtuhumiwa na SP Latifa.

Wakili Tesha akamuhoji kwamba anataka mahakama iifanye nini Tape hiyo akajibu kuwa ipokelewe kama kilelezo.

Kibatala alisimama na kuomba mahakama hiyo isiipokee tape hiyo kama kielelezo kwa kuwa utaratibu uliotumika umekinzana na sheria ya ushihidi ambapo amedai ushahidi wa tape ni ushahidi ni wa kieletroniki ambao haujajitosheleza kwenye uwasiliwashwaji wake.

“Tulitegemea wakati shahidi anaongozwa angetueleza kuwa wakati anakwenda kurekodi kamare yake aliichaji au ilikuwa na chaji na hakueleza kama wakati anarekodi kamera hiyo ilikuwa ikifanya kazi vizuri au la.”

Katika hoja nyengine Kibatala amedai sheria ya ushahidi wa kieletroni kwenye kurekodi mpiga picha anatakiwa asiwe kwenye upande wenye maslahi na kesi hiyo ambapo ameeleza shahidi huyu yupo chini ya Mwendesha mashtaka wa Serikali DPP.

Hoja nyengine Kibatala amesema kuwa kuwasilisha ushahidi wa kieletroki unapaswa kuwasilishwa kwa kiapo juu ya ushahidi huo na kwamba upande wa Jamhuri ulipaswa kueleza kwenye maelezo ya mwenendo wa mashtaka (Commito).

Baada ya wasilisho hilo Wakili Tesha alijibu hoja hizo pingamizi kwa kudai kuwa shahidi huyo hakufanya kazi chini ya DPP alitekeleza majukumu yake chini ya Mkurugenzi wa Upelelezi pia amedai kuwa hitajio la kiapo linaulazima kwenye kesi za jinai na sio kwenye kesi za jinai.

Baada ya mchuano mkali wa kisheria Jaji Kakolaki ameahilisha shauri hilo hadi kesho Jumaano tarehe 9 Machi 2022 saa tatu asubuhi atatolea uamuzi pingamizi hilo.

error: Content is protected !!