September 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mwanamke wa kwanza duniani aponywa Ukimwi kwa kupandikizwa seli

Spread the love

 

WANASAYANSI jana Jumatano tarehe 16 Februari 2022, wametangaza ufanisi wao wa kumponya mwanamke wa kwanza aliyekuwa anaishi na Virusi Vya Ukimwi (VVU), baada ya kumpandikiza seli za shina za damu (stem cell transplant). Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea)

Mwanamke huyo ambaye pia alikuwa anaugua saratani ya damu, alipandikizwa seli hiyo kutoka kwa mfadhili ambaye kwa asili alikuwa na virusi sugu vya VVU.

Tangu apandikizwe seli hiyo, mwanamke huyo kila alipopimwa hakupatikana tena na VVU kwa muda wa miezi 14.

Kesi hiyo, iliyowasilishwa jana katika Kongamano la Virusi vya Ukimwi na Maambukizi mjini Denver nchini Marekani, ilikuwa ya kwanza kuhusisha damu ya chembe hai za mama kutibu saratani ya damu ambayo ni mbinu mpya zaidi inayoweza kufanya matibabu kupatikana kwa watu wengi zaidi.

“Hii sasa ni ripoti ya tatu ya tiba katika mazingira haya, na ya kwanza kwa mwanamke anayeishi na VVU,” Sharon Lewin ambaye ni Rais Mteule wa Jumuiya ya Kimataifa ya UKIMWI.

Katika taarifa aliyoitoa kwa umma, Lewin amesema visa viwili vya awali vilitokea kwa wanaume, mmoja mwenye asili ya mzungu na mwingine Latini ambao walikuwa wamepokea seli shina za watu wazima, ambazo hutumiwa mara kwa mara katika upandikizaji wa uboho.

Kesi hiyo ilikuwa sehemu ya uchunguzi mkubwa wa Marekani kwa watu wanaoishi na VVU ambao walikuwa wamepokea aina moja ya kupandikiza damu kutibu saratani na magonjwa mengine sugu.

error: Content is protected !!