Thursday , 28 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Mkangwa: Wanahabari jiungeni vyama vya wafanyakazi
Habari Mchanganyiko

Mkangwa: Wanahabari jiungeni vyama vya wafanyakazi

Spread the love

KAMISHNA wa Kazi, Suzana Mkangwa ametoa rai kwa waandishi wa habari nchini kujiunga kwenye vyama vya wafanyakazi, ili kuhakikisha wanakuwa na nguvu ya pamoja kwenye kudai na kupigania haki zao.

Aidha, amesema ofisi yake inajiandaa kuzunguka kwenye vyombo vya habari vyote nchini ili kujiridhisha kuwa Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini inatekelezwa kwenye vyombo hivyo. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Kamishna Mkangwa amesema hayo leo tarehe 17 Febrauri, 2022 jijini Dodoma katika kikao kazi cha wadau wa sekta ya habari cha mashauriano kuhusu utekelezaji wa sheria ya ajira na mahusiano kazini.

Amesema wameamua kukutana na sekta ya habari ili kujadiliana na kushauriana namna ya kutatua changamoto zinazowakabili kama kutofuata sheria ya ajira na mahusiano kazini.

Mkangwa amesema pamoja na changamoto hizo, pia mwitikio wa waandishi kujiunga na vyama vya wafanyakazi umekuwa mdogo hivyo kuwataka watumie vyama hivyo kupigania haki zao.

“Niwaombe wanahabari jiungeni vyama vya wafanyakazi ambavyo vinasimamia sekta yenu, hivyo ndio vyombo sahihi ambavyo Serikali inataka kufanya navyo kazi kuhakikisha haki zenu za ajira zinatekelezwa kwa mujibu wa sheria ya ajira na mahusiano kazini,” amesema.

Kamishna amesema ofisi yake inajipanga kuzunguka kwenye vyombo vyote, kubaini vinavyofuata sheria ya ajira na mahusiano kazi na zile zisizofuata ili waweze kuchukua hatua stahiki.

Mkangwa amesema wamiliki wa vyombo vya habari kote nchini wanapaswa kuendesha vyombo vyao kwa mujibu wa sheria zote za nchi ikiwemo ya ajira na mahusiano kazini.

“Hatutakubali kuona mtu ameanzisha chombo cha habari halafu hatoi mikataba ya ajira, hapeleki michango ya hifadhi ya jamii, bima ya afya na mingine, hili halikubaliki, naomba waajiri mbadilike,” amesema.

Kamishna amesema ofisi yake itashirikiana na wizara ya habari, mawasiliano na teknlojia ya habari kuhakikisha wanafikia kila chombo.

Aidha, Kamishna amewataka waajiri kurusu wafanyakazi kujiunga na vyama vya wafanyakazi, kuchangia na kufanya mikutano sehemu za kazi.

Kwa upande wake Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Profesa Jamal Katundu amewataka waajiri kuboresha mahusiano kazini ili kupunguza migogoro inayotokea mahali pa kazi.

Amesema sekta ya habari ni sekta muhimu katika kuchangia uchumi wa nchi na Serikali ina wajibu wa kuweka mazingira mazuri kwa wawekezaji pia wajibu wa kuhakikisha wanalinda haki za wafanyakazi.

Katundu amesema migogoro inayojitokeza kati ya mwajiri na mwajiriwa inaweza kumaliza kwa mashauriano .

“Hapo ndio kuna umuhimu wa mwajiri na mwajiriwa kuboresha mahusiano ili kupunguza majukumu ya kusikiliza migogoro inayojitokeza,” amesema.

Amesema ili kuondoa misuguano kati ya mwajiri na Serikali lazima kusimamia kwenye haki.

Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari (Maelezo) Rodney Mbuya ameitaka sekta ya habari kutumia teknolojia kuhakikisha sekta inakuwa na kuchochea maendeleo nchini.

“Sekta ya habari ni nguvu laini, tuone tumewekeza na kuajiriwa katika sekta muhimu na ina mchango mkubwa katika uchumi na maendeleo,” amesema.

Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Vyombo vya Habari Tanzania (JUWUTA), Selemani Msuya aliwataka waandishi wa habari kuungana pamoja ili kufanikisha kudai haki zao.

Msuya aliviomba vyombo vya habari kutoa mikataba kwa waandishi wote ili kuhakikisha wananufaika na haki mbalimbali anazopata mwajiriwa kama bima ya afya na mafao.

Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha wafanyakazi, Watafiti, Wanataaluma na Washiriki wake (RAAWU), Jane Mihanji amesema kumekuwa na changamoto kubwa katika kutengeneza ajira za waandishi wa habari.

Amesema wamiliki wa vyombo vya wahabari wamekuwa wakitumia jina la ‘waandishi wa kujitegemea ‘ ili kuminya haki zao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyabiashara, wawekezaji China waridhia kuwekeza bil. 800 katika sekta 5 nchini

Spread the loveUJUMBE wa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Jimbo la Changzhou...

Habari Mchanganyiko

Bil. 4.42 kumaliza uhaba maji kata 2 Musoma Vijijini

Spread the loveWANANCHI wa kata za Busambara na Kiriba, Jimbo la Musoma...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Soko nepi za watoto lashuka, watu wazima lapaa

Spread the loveKiwanda cha kutengeneza nepi cha Japan kimetangaza kuwa kitaacha kutengeneza...

error: Content is protected !!