October 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mwanajeshi feki kijana anaswa

Spread the love

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limemkamata mwanajeshi feki aliyekuwa akitumia sare za jeshi hilo kufanya uhalifu. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe mosi Februari mwaka 2019 Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro  Mambosasa ameeleza kuwa Emmanuel Magoti (18) amekamatwa na suruali mbili, koti na fulana mbili za  JWTZ.

“Mnamo tarehe 30 January 2019 majira ya saa nane mchana huko maeneo ya Mbagala Jeshi la Polisi lilifanikiwa kumkamata kijana huyo baada ya kupata taarifa kutoka kwa Polisi Jeshi (MP) kuwa, kuna kikundi cha vijana kinachofanya uhalifu kwa kutumia sare za JWTZ” ameeleza Mambosasa.

Amesema kuwa, askari wa jeshi hilo wakishirikiana na  Polisi Jeshi (MP) walifika katika nyumba ya mtuhumiwa na kufanikiwa kukamata sare hizo.

“Mtuhumiwa katika mahojiano alikiri kujihusisha na vitendo vya uhalifu akishirikiana na wenzake wawili katika maeneo mbalimbali ya Mbagala.”

Amesema pia mtuhumiwa huyu anakiri kuwa alikuwa mfungwa katika gereza la Segerea kwa kosa la wizi na kuwa aliachiwa kwa msamaha wa raisi 2018.

Msako mkali unaendelea wa kuwatafuta wenzake wawili anaoshirikiana nao katika matukio hayo.

Wakati huo huo Kamanda Mambosasa ameeleza kuwa jeshi hilo limekamata watu tisa wanaohusika na mtandao wa wizi wa pikipiki jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa, jeshi hilo silku ya tarehe 2 Januari liliwatia mbaroni watu 02/01/2019 huko maeneo ya Gongo la Mboto uliwekwa mtego ambao ulifanikiwa kuwakamata wanawake wawili Fatuma Salum na Halima Revocutus

“Watuhumiwa hao ambao katika mahojiano ya awali walikiri kuhusika katika matukio mbalimbali ya unyang’anyi wa pikipiki na kuwa wao huagizwa kukodi pikipiki na wahalifu wenzao wa kiume kisha kufanikisha uporaji huo,” amesema.

Ameleeleza kuwa  watuhumiwa hawa waliweza kuwataja wenzao ambao hushirikiana kufanya unyang’anyi huo maeneo ya Pugu, Mombasa –Ukonga na Gongo la mboto,ambao ni :-

Emmanuel Kiabi (23)mkazi wa Kipunguni B, Yohana Anderson (18)mkazi wa Mbezi Beach, Adam Rashid (24)mkazi wa Mazizini, Haruna Kassim (25)mkazi wa Ukonga mazizini.

Wengine ni pamoja na Innocent Massawe (21)mkazi wa Gongo la mboto Mzambarauni na Daniel Dangod (18)mkazi wa Mazizini Ukonga.

Kamanda Mambosasa amesisitiza kutoa tahadhari kwa wanancho juu ya wizi na matapeli wa mtandao wa simu.

“Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limekuwa likipokea malalamiko kutoka kwa wananchi wakidai kupokea jumbe fupi za maandishi zinazowashawishi kutuma fedha ama kufanya malipo ya kifedha kwa njia ya mtandao.

Amesema kuwa, jeshi hilo lipo macho na tayari limeanza kuwatia mbaroni wahalifu hao.

error: Content is protected !!