Friday , 3 May 2024
Home Kitengo Biashara Mwana FA anogesha Tamasha la Exim Bima Festival
BiasharaMichezo

Mwana FA anogesha Tamasha la Exim Bima Festival

Spread the love

NAIBU Waziri Wa Utamaduni, Sanaa Na Michezo, Hamis Mwinjuma ‘Mwana FA’, mwishoni mwa wiki alipamba  msimu wa kwanza wa Tamasha la Bima Festival lililoratibiwa na benki ya Exim Tanzania na kutoa wito kwa kampuni za bima na taasisi za fedha nchini kuongeza ufadhili wao kwenye sekta ya michezo ili kuchochea zaidi kasi ya ukuaji wa sekta hiyo inayokua kwa kasi. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Naibu Waziri Wa Utamaduni, Sanaa Na Michezo, Hamis Mwinjuma (Mwana FA) akipiga penati kuashiria uzinduzi rasmi wa msimu wa kwanza wa Tamasha la Exim Bima Festival la benki ya Exim Tanzania lililofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Tamasha hilo liliandaliwa kwa ushirikiano na wadau mbalimbali wa sekta ya bima nchini zikiwemo kampuni mbalimbali za bima nchini. Wanaoshuhudia ni pamoja na Mkuu wa Idara ya Uwekezaji Kimkakati na Matawi ya Nje wa benki ya Exim Tanzania, Sumit Shekhar (kulia)

Zaidi Mwinjuma aliziomba taasisi hizo kubuni huduma mbalimbali zinazolenga kuwasaidia wadau wa sekta ya michezo na burudani nchini.

Katika tamasha hilo lililoratibiwa  kwa ushirikiano na wadau mbalimbali wa sekta ya bima nchini zikiwemo kampuni za Alliance life Assurance Limited, Alliance Insurance Corporation Limited, Jubilee Allianz General Insurance Company Limited na Strategis Insurance Company Limited.

Kampuni nyingine ni The Heritage Insurance Tanzania na kampuni wateja wa benki hiyo ikiwemo kampuni ya bidhaa za plastic ya CELLO pamoja na kampuni ya uchimbaji madini ya Taifa Mining, ilishuhudiwa timu ya mpira wa miguu ya Exim ikiibuka mshindi wa jumla kwenye mashindano ya mpira wa miguu yaliyohusisha wadau wote.

Akizungumza wakati akizindua tamasha hilo Naibu Waziri Mwinjuma pamoja na kuwapongeza wadau hao kwa kuandaa tukio hilo lililotoa fursa ya kufurahia pamoja,  kubadilishana mawazo na kujengeana ufahamu zaidi kuhusu huduma zao.

Naibu Waziri Wa Utamaduni, Sanaa Na Michezo, Hamis Mwinjuma (Mwana FA) (Kushoto) akizungumza na wadau mbalimbali wa sekta bima nchini walioshiriki kwenye Tamasha la Exim Bima Festival lililoratibiwa na benki ya Exim Tanzania mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Wanaomsikiliza ni pamoja na Mkuu wa Idara ya Uwekezaji Kimkakati na Matawi ya Nje wa benki ya Exim Tanzania, Sumit Shekhar (wa pili kushoto), Mkuu wa Kitengo cha Mikopo Benki ya Exim, Zainab Nungu (katikati), Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano, Stanley Kafu (wa pili kulia) na Mkuu wa kitengo cha Usimamizi wa Mali za benki ya Exim, Queen Siraki (kulia)

Pia aliwasihi wajitokeze zaidi kuunga mkono shughuli mbalimbali zinazofanywa na wadau wa michezo na burudani nchini kwa kudhamini shughuli zao mbalimbali na kuwatumia kwenye hamasa za kibiashara yakiwemo matangazo.

“Mchango wenu unaweza kutafsiriwa katika maeneo mengi ya kimichezo lakini msisitizo wangu nauweka zaidi katika udhamini wa matukio mbalimbali ya michezo husani katika uibuaji wa vipaji na kusaidia vilabu mbalimbali vinavyoshiriki ligi mbalimbali hapa nchini ikiwemo ligi Kuu.

“Zaidi pia niwaombe muendelee kubuni huduma za bima na huduma za kifedha mahususi kwa wanamichezo na wasanii ili muwasaidie kulinda afya na kazi zao na zaidi kuwajenga kiuchumi,’’ alisema.

Zaidi Mwinjuma aliipongeza benki hiyo kwa jitihada zake za kukuza michezo hapa nchini kupitia msaada wa vifaa vya michezo inavyotoa kwa shule za msingi na sekondari katika mikoa mbalimbali hapa nchini.

“Mmeonyesha dhamira na nia njema ya kuinua vipaji vya vijana na kuwezesha maendeleo ya michezo nchini. Tunatambua mchango wenu mkubwa katika kuendeleza michezo na tunawashukuru kwa kuwa wabia wetu katika kufanikisha malengo yetu ya kitaifa katika sekta hii,” alisema.

Alisema huku pia akionesha matumaini makubwa kuwa tamasha la Exim Bima Festival litakuwa na mafanikio makubwa na litaleta matunda yaliyotarajiwa.

Mkuu wa Idara ya Uwekezaji Kimkakati na Matawi ya Nje wa benki ya Exim Tanzania, Sumit Shekhar (aliyesimama) akizungumza na wadau mbalimbali wa sekta bima nchini walioshiriki kwenye Tamasha la Exim Bima Festival lililoratibiwa na benki hiyo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Wanaomsikiliza ni pamoja na Naibu Waziri Wa Utamaduni, Sanaa Na Michezo, Hamis Mwinjuma (Mwana FA) (kushoto)

Awali, akizungumza kwa niaba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim, Mkuu wa Idara ya Uwekezaji Kimkakati na Matawi ya Nje wa benki hiyo, Sumit Shekhar, alisema kupitia tamasha hilo litakalokuwa likifanyika kila mwaka.

Alisema benki hiyo imejipanga kutumia vema fursa  ya michezo na burudani kuboresha mahusiano yake na wadau wake mbalimbali wakiwemo wateja, wadau wa bima, wafanyakazi, mamlaka mbalimbali zinazosimamia sekta ya bima na benki pamoja na serikali.

Timu ya ushindi! Kikosi cha timu ya Benki ya Exim kilichoibuka mshindi wa jumla kwenye mashindano ya mpira wa miguu yaliyohusisha wadau wote.

“Tukiwa kama wadau muhimu wa sekta ya fedha na bima nchini kupitia huduma yetu ya Bima ijulikanayo kama ‘Bima tu Malipo Tuachie’ tumejipanga kuhakikisha tunalitumia vema tamasha hili kama mkakati muhimu wa kuboresha mahusiano baina yetu na wadau wetu tukiamini mahusiano ndio nguzo ya kwanza kwenye biashara yoyote na tamasha la Exim Bima Festival linakuja kama namna bora ya kutusaidia kufanikisha hilo,’’ alisema Shekhar.

Akizungumzia ushindi wa jumla katika mashindano ya mpira wa miguu baina ya wadau hao, mfungaji bora katika mashindano hayo, Calvin Kilua kutoka timu ya benki ya Exim alisema siri ya mafanikio ni timu yake kujiandaa vema kwa ajili mashindano hayo sambamba na kutafsiri vema maelekezo ya kocha wa timu hiyo ambae ni Meneja Rasilimali Watu Bw Mikidadi Ngoma.

“Baada ya mafanikio haya tunaamini kwamba tamasha lijalo litahusisha timu nyingi zaidi na ushindani utaongezeka.

“Hivyo tutaendelea kujiweka sawa kwa mazoezi zaidi kwa kuwa mazoezi pia ni afya na ukizungumzia afya ni moja ya agenda ya msingi kwenye huduma zetu za bima,’’ alisema Stanley Kafu, Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa benki ya Exim.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yashiriki maadhimisho Mei Mosi Arusha

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeungana na maelfu ya...

Michezo

Europa na Conference kukupatia pesa ndefu leo

Spread the love  ALHAMISI ya leo tutaenda kushuhudia mitanange ya kukata na...

Biashara

Promosheni ya bil 1 kutoka Meridianbet kasino, cheza na ushinde zawadi kubwa

Spread the love  INGIA katika ulimwengu wa zawadi za kushangaza: Jishindie sehemu...

error: Content is protected !!