Friday , 1 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Mchimba madini jela maisha kwa kubaka, alihonga Sh 500
Habari Mchanganyiko

Mchimba madini jela maisha kwa kubaka, alihonga Sh 500

Spread the love

Mahakama ya wilaya ya Songwe imemtia hatiani na kumhukumu kifungo cha maisha gerezani mshtakiwa Dickson Mbadame (32) – mchimbaji wa madini kwa kosa la kubaka. Anaripoti Ibrahim Yassin, Songwe…(endelea).

Mbadame alikamatwa tarehe 29 Mei 2023 maeneo ya Mkwajuni ambapo inadaiwa kuwa alimrubuni mwanafunzi wa darasa la nne mwenye umri wa miaka tisa kwa kumpa fedha kiasi cha Sh 500.

Akitoa hukumu hiyo mwishoni mwa wiki katika kesi namba 36 ya mwaka 2023, Hakimu mkazi wa wilaya ya Songwe, Agustino Lugome amesema mahakama imejiridhisha pasipo na shaka kutokana na ushahidi uliotolewa na upande wa Jamhuri na kumtia hatiani mtuhumiwa huyo.

Amedai mshtakiwa amehukumiwa kifungo hicho ili iwe fundisho kwa watu wengine wanaojihusisha na vitendo vya ukatili wa kijinsia dhidi ya watoto ambao wanawaharibia ndoto zao za maisha.

Nje ya mahakama, badhi ya wananchi waliohudhuria mahakamani hapo walisema kuwa hukumu hiyo itawafanya mafataki wenye tabia ya kuharibu wanafunzi, kuwa fundisho kwao

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Karafuu, Parachichi yawa fursa Morogoro

Spread the loveIMEELEZWA kuwa zao la karafuu ambalo kwa sasa linalimwa pia...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Washindi 12 NMB MastaBata na wenza wao wapaa Afrika Kusini

Spread the loveWASHINDI 12 wa kampeni ya kuhamasisha matumizi yasiyohusisha pesa taslimu...

Habari Mchanganyiko

4 wanusurika kifo ajali ya ndege Serengeti

Spread the loveWATU wanne wakiwamo abiria watatu na rubani mmoja wamenusurika kifo...

Habari Mchanganyiko

Mafua yamtesa Papa, afuta mikutano

Spread the loveKiongozi wa Kanisa katoliki duniani, Papa Francis amelazimika kufuta mkutano...

error: Content is protected !!