Wednesday , 8 February 2023
Home Kitengo Maisha Elimu Musoma Vijijini wafanya harambee posho za walimu, ujenzi wa sekondari
Elimu

Musoma Vijijini wafanya harambee posho za walimu, ujenzi wa sekondari

Spread the love

 

WAKAZI wa Jimbo la Musoma Vijijini, wakiongozwa na Mbunge wao, Profesa Sospeter Muhongo, wamefanya harambee ya kuchangisha fedha za kukamilisha ujenzi wa miundombinu ya shule mpya ya Sekondari Bwai, mkoani Mara. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mara … (endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Ijumaa tarehe 20 Januari, 2023 na Ofisi ya Mbunge wa Musoma Vijijini, harambee hiyo imefanyika jana tarehe 19 Januari 2023, ikiongozwa na Prof Sospeter Muhongo .

“Harambe imefanyika ya ukamilishaji wa vyumba vitatu vya madarasa, kwa sasa vyumba vilivyokamilika na vinatumika ni vitatu. Ujenzi wa choo kipya chenye matundu manne, kwa sasa kipo choo chenye matundu manane,”

“Ujenzi wa jengo la utawala ambalo msingi wake umekamilika. kwa sasa, ofisi ya walimu ni chumba kimoja cha darasa. Ujenzi ni endelevu, na michango ni endelevu hadi hapo miundombinu muhimu itakapokamilika, ikiwemo, maabara tatu za masomo ya sayansi, maktaba, nyumba za walimu, viwanja vya michezo,” imesema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imetaja michango iliyopatikana katika harambee hiyo ambayo ni endelevu, ikiwemo saruji mifuko 51 iliyotolewa na wananchi pamoja na mifuko mingine 100 iliyotolewa na Prof. Muhongo.

Pia, wananchi walichanga misumari kilo tatu, fedha taslimu kiasi cha Sh. 610,000 na nguvu kazi ya kujenga miundombinu hiyo, huku Prof. Muhongo akichangia mabati bando mbili zenye jumla ya mabati 24.

Kwenye harambee ya kupata walimu, wazazi wamekubali kuchangia Sh. 3,000 kila mwezi, pamoja na kuajiri walimu wa kujitolea kwa posho ya Sh. 200,000 kila mwezi, huku Prof. Muhongo akiahidi kuchangia Sh. 100,000 kwa kila mwalimu kwa mwezi , ambao wako watatu (jumla Sh. 300,000).

Taarifa hiyo imeeleza zaidi kuwa, Prof. Muhongo ametoa makasha manne ya vitabu kwa sekonda hiyo mpya yenye kidato kimoja.

Kwa sasa shule hiyo ina walimu watano akiwemo Mkuu wa Shule, lakini haina walimu wa masomo ya Kingereza, hesabu na fizikia.

Shule ya Sekondari Bwai ina wanafunzi 125 kati ya 153 ambao wanatakiwa kuanza masomo yao ya kidato cha kwanza.

“Vilevile, shule hiyo mpya, iitwayo Bwai Sekondari, itapunguza mirundikano ya wanafunzi kwenye madarasa ya Sekondari ya Kiriba,” imesema taarifa hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

ElimuHabari Mchanganyiko

Waliopata Division one St Anne Marie Academy waula, Waahidiwa kupelekwa Ngorongoro, Mikumi

Spread the love WANAFUNZI wa shule ya St Anne Marie Academy waliofanya...

ElimuMakala & Uchambuzi

Waraka maalumu kwa NECTA, “hawapaswi kuungwa mkono”

Spread the loveHATUA iliyotangazwa na Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA), ya...

Elimu

NACTVET yafungua dirisha la udahili

Spread the love  BARAZA la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo...

Elimu

Prof. Mwakalila awafunda wanafunzi Chuo Mwalimu Nyerere, “ulipaji ada ni muhimu”

Spread the love  MKUU wa Chuo cha Kumbukumbu cha Mwalimu Nyerere (MNMA),...

error: Content is protected !!