Sunday , 5 February 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Mwenezi mpya CCM aanza na vishikwambi kwa walimu
Habari za Siasa

Mwenezi mpya CCM aanza na vishikwambi kwa walimu

Spread the love

 

KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Sophia Mjema, ametoa wiki moja kwa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, kuhakikisha walimu wote nchini wanapata vishikwambi vilivyotolewa na Serikali kwa ajili ya kuimarisha ufundishaji shuleni. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Dk. Mjema ametoa agizo hilo jana Alhamisi, akisema kwamba litaanza kutekelezwa ndani ya wiki moja kuanzia leo tarehe 20 Januari 2023.

“Ulitengwa muda maalumu wa kutolewa kwa vishikwambi hivi ambao ulikuwa unaishia Januari 15, mwaka huu, lakini Chama kimepokea malalamiko kwamba hadi leo kuna baadhi ya makundi hayajapata hivyo vishikwambi. Lakini pia kuna baadhi ya wilaya hawajagawa kabisa vishikwambi hivyo,” amesema Dk. Mjema na kuongeza:

“Kuna maeneo mengine unakuta walimu wako 10 na wote wanahitaji na wanastahili kupata, lakini unakuta vishikwambi vinatoka vinane wawili wanaachwa. Chama kinatoa maelekezo, kinaielekeza wizara husika (Wizara ya Elimu) kuhakikisha zoezi hili linakamilika na walengwa wote wanaostahili kuhakikisha wameipata vishikwambi hivyo,”

“Lakini si hivyo tu bali pia wahakikishe malalamiko haya hayapo na wasimamie zoezi kuona makundi yaliyopaswa kupewa yanafikiwa na wale ambao hawajapata wapate. Baada ya wiki moja tupate taarifa zoezi hili limekwendaje.”

Serikali iliagiza vishikwambi vilivyokuwa vinatumika katika zoezi la Sensa ya Watu na Makazi la Agosti mwaka jana, visambazwe kwa walimu wote nchini kabla ya tareje 15 Januari 2023.

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Juma Kipanga, alisema vishikwambi vilivyotumika wakati wa sensa vilikuwa 6,600 na kwamba Serikali imeongeza vishikwambi vingine zaidi ya 100,000 ambavyo vitakwenda kugawiwa kwa walimu, wadhibiti ubora.

Dk. Mjema ametoa agizo hilo ikiwa zimepita siku sita tangu ateuliwe na Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kuchukua mikoba ya Shaka Hamdu Shaka, tarehe 14 Januari 2023.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo aungana na wananchi ujenzi maabara za sekondari

Spread the loveMBUNGE wa Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo, kwa kushirikiana na...

Habari za Siasa

CCM apiga marufuku wazazi kuwatumia watoto wa kike kwenye mambo ya kimila

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Daniel Chongolo...

Habari za Siasa

Ofisi za mabalozi wa mashina zitumike kuwale vijana kimaadili – Chongolo

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo ameagiza...

Habari za Siasa

Vijana ACT-Wazalendo Dar wampa tano Rais Samia

Spread the love  NGOME ya Vijana ya Chama cha ACT-Wazalendo, kimempongeza Rais...

error: Content is protected !!