Thursday , 25 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Mshindi NMB MastaBata Kote-Kote akabidhiwa pikipiki
Habari Mchanganyiko

Mshindi NMB MastaBata Kote-Kote akabidhiwa pikipiki

Spread the love

MSHINDI wa kampeni la NMB MastaBata Kote-Kote inayoendeshwa na Benki ya NMB, Emmanuel Marumbo kutoka mkoani Tabora amekabidhiwa rasmi Pikipiki yake aina ya Boxer. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Mshindi huyo aliyepatikana katika droo ya saba ya kamoeni hiyo iliyofanyika mkoani Tanga, amekabidhiwa zawadi yake na Meneja Mauzo wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi, Trifon Malkiory.

Meneja Masoko NMB Kanda ya Magharibi, Trifon Malkiory (wapili kushoto) akimkabidhi kadi ya Pikipiki Mshindi wa kampeni ya NMB MastaBata Kote-Kote wiki iliyopita Emmanuel Marumbo (wapili kulia) kutoka Mkoani Tabora, katika hafla ya kukabidhi zawadi hiyo iliofanyika katika Benki hiyo tawi la Mihayo Mjini Tabora. (kulia) kaimu Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Mihayo, Prudence Rwegasira na kushoto ni Afisa muandamizi wa biashara ya kadi wa Benki hiyo, Said Kiwanga.

Hafla ya kumkabidhi zawadi hiyo imefanyika jana Ijumaa, tarehe 20 Januari 2023, kwenye Tawi la NMB Mihayo mjini Tabora, ambapo kabla ya kumkabidhi zawadi mshindi Meneja huyo aliendesha droo ya tisa ya kamoeni hiyo kwa wiki hii.

Katika droo hiyo iliyosimamiwa na Mkaguzi kutoka Bodi ya michezo ya kubahatisha, Goodluck Msomigulu, amepatikana Aidan Stephen Lukindo kutoka Mkoani Morogoro na kuwa mshindi wa wiki hii na kujinyakulia zawadi ya Pikipiki aina ya Boxer.

Aidha, droo hiyo imewapata washindi wengine 75 ambao wamejishindia kiasi cha Sh100,000 kila mmoja.

Meneja Masoko Trifon amesema kuwa NMB imekuwa ikiendesha hiyo kwa miaka minne tangu kuanza kwake huku likilenga kuhamasisha wateja wake kutumia NMB Mastercard na Mastercard QR (lipa Mkononi).

Amesema NMB inaendesha kampeni hiyo ikiwa ni njia ya kurejesha faida kwa wateja wake, ambapo washindi ujishindia zawadi mbalimbali zikiwemo fedha taslimu, pikipiki pamoja na safari ya kuelekea Dubai kwa siku nne kwa droo ya mwisho kabisa.

“Niwakumbushe pia zaidi ya Sh. Milioni 300 zimetengwa kama zawadi kwa washindi 854, na kampeini inaendeshwa ndani ya wiki kumi na kila wiki washindi 75 wanapokea kiasi cha sh. 100,000 na mshindi mmoja pikipiki” amesema Malkiory.

Amewataka wateja wa Benki hiyo kuendelea kutumia kadi zao za NMB Master Card, siyo tu kwa ajili ya kutolea pesa kwenye mashine za ATM bali hata kwa matumizi mbalimbali ili wajishindie zawadi mbalimbali kupitia kamoeni ya NMB Mastabata kotekote.

“Wateja wetu wanaweza kufanya malipo ya skani QR kwa kulipa mkononi katika sehemu za migahawa, supermarket, vituo vya mafuta lakini pia hata kwenye sehemu za starehe na hata kuagiza bidhaa mbalimbali kupitia mitandao” amesema Malkiory.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa zawadi ya Pikipiki mshindi wa droo ya wiki iliyopita, Emmanuel Marumbo amesema mwanzoni hakuamini kama kweli ameshinda zawadi hiyo licha ya kuwashirikisha wenzake.

Amesema amekuwa ni mtu wa kutumia kadi ya benki yake kwa ajili ya manunuzi ya vitu mbalimbali, huku akibainisha kuwa huwa hatembei na pesa taslimu bali ufanya manunuzi kwa kutumia kadi yake.

Ameishukuru benki ya NMB kwa zawadi waliyompatia huku akibainisha kuwa itamsaidia katika shughuli zake za biashara za kila siku anazozifanya, kwani amepata usafiri wa kurahisisha kazi zake.

Amewataka wateja wa NMB kujiwekea utaratibu wa kufanya malipo mbalimbali kwa kutumia kadi za benki, kwani kufanya hivyo kuna usalama zaidi wa pesa lakini pia NMB kupitia Mastabata, inatoa zawadi mbalimbali.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!