Sunday , 19 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi
Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza, SACP Wilbroad Mutafungwa
Spread the love

JACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza, kwa tuhuma za kumchoma visu hadi kumuua mke wake, Mariam Ulacha (42), chanzo kikiwa na wivu wa mapenzi akimtuhumu kuwa na mahusiano na wanaume wengine mahali wanapoishi wilayani Buchosa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mwanza…(endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mwanza, Wilbroad Mutafungwa, amedai mtuhumiwa alifanya mauaji hayo baada ya kuzozana na marehemu mke wake usiku kucha, kisha asubuhi kuamua kumchoma visu mwilini kitendo kitendo kilichofanya Mariam kuvuja damu hadi kupoteza maisha.

“Mwanaume huyo mkatili alimuuwa mke wake kwa kumchoma visu mwilini mara kadhaa jambo ambali lilipelekea mwanamama huyo kuvuja damu nyingi na hatimaye kupotez amaisha.Chanzo ni wivu wa mapenzi kwa sababu siku moja kabla ya mauaji hayo mwanaume alianza kumtuhumu mwanamke kwa kuwa na mahusiano na wanaume wengine hapo kijijini hali iliyoleta mzozo usiku kucha hatimaye asubuhi akafanya ukatili wake,” amesema Kamanda Mutafungwa.

Kamanda Mutafungwa amesema, baada ya mtuhumiwa kugundua anafuatiliwa kila kona, mnamo tarehe 13 Aprili 2024, aliamua kujisailimisha kwenye Kituo cha Polisi Buchosa.

“Baada ya msako kuwa mkubwa kila eneo analoenda anakuta watu wamejipanga kumkamata aliamua kwenda kujisalimisha kituo cha polisi. Askari wetu waliokuwa kituoni Buchosa walimkaribisha kwa kumfunga pingu na kumueweka chini ya ulinzi ambapo sasa hivi anaendelea kuhojiwa,” amesema Kamanda Mutafungwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

CCM yamteua Pele kuwa mgombea ubunge Kwahani

Spread the loveKamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Canada yatenga bilioni 38 kutekeleza mradi ya kuinua vijana TZ

Spread the loveSERIKALI ya Canada kupitia ‘CARE International Canada’ imetenga takribani Sh...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Ujenzi kituo cha kupoza umeme Chalinze wafikia asilimia 93.7

Spread the loveKamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imeeleza...

Habari Mchanganyiko

Balile ateuliwa rais wa wahariri Afrika Mashariki

Spread the loveJumuiya ya Wahariri wa Afrika Mashariki (EAES), imemchagua Mwenyekiti wa...

error: Content is protected !!